Thursday, January 21, 2016

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA CCM CALIFORNIA.

https://encrypted-tbn3.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcSiwNqnpMFp1tAdcL3jhSJn2AomV2hxCF3Bfz1RgGywHlUjangu
Chama cha mapinduzi- Tawi la California, tunapenda kutoa salamu za pole zilizojaa masikitiko makubwa kwa familia na ndugu wa Marehemu wa Mwenyekiti wa Tawi la CCM la DMV Mzee George Sebo. Pia tunapenda kutoa pole kwa uongozi wa chama wa tawi la DMV kwa kuondokewa na kiongozi wao mahili. Lakini pia tunapenda kutoa pole kwa watanzania wote wa DMV na wengine wote waliomjua marehemu.
Tumesikitishwa na kuguswa sana na huu msiba hasa kwa kumjua marehemu kwa ukaribu sana, kwa mapenzi yake kwa watu wote na nchi yake. Wengi wetu huku northern California wanaccm na wasio wanaccm tunamjua marehemu kwa ukaribu kwani alikuwa akitutembelea huku mara kwa mara na kuna kipindi yeye na mke wake walikuwa wanachama wa jumuiya yetu ya watanzania waishio hapa bay area. Hivyo ni mtu wetu tunafahamu fika.
Kama chama tutamkumbuka sana kwa kuwa mzee wa ushauri katika chama chetu na matawi yetu hapa Marekani. Tutayazingatia yale yote aliyotuachia na kuyafanyia kazi.

Tunaomba mungu wa rehema aiweke roho yake mahala pema peponi. AMINA
Erick Byorwango

Karibu-Tawi la California.

No comments: