Friday, January 22, 2016

Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika yahimiza ushirikishwaji wa Wanawake katika Ngazi za Maamuzi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) kutoka Afrika Kusini akiongea na Wajumbe (hawapo pichani) waliohudhuria Warsha ya siku mbili kujadili namna ya kuwashirikisha Wanawake katika ngazi za maamuzi leo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika Mbunge toka Afrika Kusini Mhe. Angella Didiza akichangia mada wakati wa Warsha ya siku mbili kujadili namna ya kuwashirikisha Wanawake katika ngazi za maamuzi leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Msaidizi Wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kutoka Tanzania, Bwana Demetrius Mgalami akichangia mada wakati wa Warsha ya siku mbili kujadili namna ya kuwashirikisha Wanawake katika ngazi za maamuzi leo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria Ufunguzi wa Warsha ya ya siku mbili ya kujadili namna ya kuwashirikisha Wanawake katika ngazi za maamuzi wakifuatilia hotuba za Viongozi leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) kutoka Afrika Kusini (aliyekaa katikakati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe waliohudhuria Warsha ya siku mbili kujadili namna ya kuwashirikisha Wanawake katika ngazi za maamuzi leo jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Benedict Liwenga)
 
Na Benedict Liwenga.
Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika(Commonwealth Parliamentary Association Africa Region Secretariat), imefanya Ufunguzi wa Warsha ya siku mbili inayowakutanisha Wabunge wa Jumuiya ya Madola, Kanda ya Afrika (Commonwealth Women Parliamentarians Africa Region) kujadili Ushiriki wa Wanawake katika Ngazi za Maamuzi iliyozikutanisha jumla ya nchi Nane za Afrika.
Akifungua Warsha hiyo leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) kutoka Afrika Kusini, ameipongeza Tanzania kwa kufanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kwa amani, uhuru na haki pasipo kumwaga damu na kuwataka nchi nyingine kuiga mfano huo.
Aidha, Mhe. Maseko ameipongeza Tanzania kwa kuonyesha juhudi za dhati za kuongeza idadi inayoridhisha ya Wabunge wanawake katika Bunge lake ikiwa ni sehemu ya kuwashirikisha wanawake katika ngazi mbalimbali za kisiasa na kijamii
“Licha kutambua majukumu ya mwanamke katika jamii, Warsha hii hainabudi kujadili masuala ya kuwashirikisha wanawake katika ngazi za maamuzi na kuongeza idadi yao katika Mabunge na kuwajengea uwezo”, alisema Maseko.
Aliongeza kuwa wanawake ambao wako katika Mabunge hawanabudi kujiskia huru katika kutekeleza majukumu yao kwani wana haki ya kushiriki katika masuala yote yakiwemoya kijamii na kisiasa.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika Mbunge toka Afrika Kusini Mhe. Angella Didiza nae ameipongeza Tanzania kwa kukubali kufanya warsha hiyo nchini ikiwa ni Makao Makuu ya Secretarieti na kuongeza kuwa kuna umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika masuala ya ngazi za maamuzi ili kubuni mbinu na mikakati ya kuongeza idadI ya Wanawake katika ngazi za siasa na kijamii.
Mhe. Didiza ameongeza kuwa, kuna masuala mbalimbali ambayo yanazihusu nchi ambazo Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika licha ya hali ya uchumi kutokuwa nzuri kwa baadhi ya nchi zetu lakini pia tunanapaswa
 “Masuala ya ulinzi na usalama yana umuhimu wake kwani tumeona matukio mbalimbali yanayohusiana na manyanyaso ya mwanamke katika masuala ya Uchaguzi na mapigano mbalilmbali katika baadhi ya nchi lakini pia tumeona jinsi baadhi ya wanawake walivyopoteza maisha yao wakitetea haki zao wakiwa wagombea”, alisema Didiza.
Aliongeza kuwa Warsha hiyo ni sehemu ya Utekekelezaji wa Mpango wa mafunzo pamoja baina ya Makao Makuu ya CPA yaliyoko Uingereza na CPA Kanda ya Afrika. Ambapo Dhima kuu ya Warsha hiyo ikiwa ni “Kuongeza Ushiriki wa Wanawake
katika Ngazi za Maamuzi”
Kwa upande wake Katibu Msaidizi Wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kutoka Tanzania, Bwana Demetrius Mgalami ameeleza kuwa kuwa kufanyikakwa warsha hiyo ni chachu ya maendeleo kwa kuwashirikisha wanawake katika ngazi mbalimbali za kisiasa na kijamii ambapo kupitia mada mbalimbali zinazowasilishwa na Wataalam kutoka Tanzania na Kenya ikiwemo Mifumo ya Uchaguzi ili kuweza kumsaidia mgombea, Sheria na taratibu mbalimbali ya masuala ya uchaguzi,Sera za Vyama vya Siasa na Akina Mama na Vyombo vya Habari.
Aidha, nchi zilizoweza kushiriki katika Warsha hiyo ni Tanzania, Uganda, Kenya, Ghana, Nigeria, Zambia, Mauritus pamoja na Afrika Kusini.

Warsha hiyo inayohudhuriwa na Waheshimiwa Wabunge Wanawake kutoka Mabunge wanachama wa CPA Kanda ya Afrika inatarajiwa kufungwa siku ya Ijumaa, Januari 22, 2016 na Spika wa Bunge la Uganda, Mhe. Rebecca Kadaga (Mb), ambae pia ni Mwenyekiti wa CWP Kimataifa.

No comments: