Baadhi ya bidhaa zilizokwisha muda wake zikiwa kwenye maandalizi ya kuteketezwa katika Dampo la Pugu Kinyamwezi jijini Dar es Salaam.
Katapila likizikanyagakanyaga kwa lengo la kuziteketeza bidhaa mbalimbali zikiwemo pampasi na dawa za meno zilizopitwa na wakati na zingine zisizo na ubora katika Dampo la Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam. Bidhaa hizo zenye thamani ya sh. mil. 20, kutoka Marekani na China zilikamatwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Na Charity James
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeteketeza bidhaa hafifu na zilizokwisha muda wake zenye thamani ya sh. milioni 20 kutoka nchini Marekani na China.
Akizungumza wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo jijiniDar es Salaam jana, Ofisa habari wa TBS, Roida Andusamile alizitaja bidhaa hizo kuwa ni dawa za meno, pampas, sabuni za kuogea na wipes.
Alisema miongoni mwa bidhaa hizo zilikuwa ni kwaajili ya kutoa msaada katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara huku nyingine zikiingizwa kwaajili ya biashara.
"Kazi ya kuteketeza bidhaa zenye ubora hafifu ni endelevu lengo letu ni kuhakikisha tunaepusha madhara kwa watumiaji ambao wanashindwa kutambua bidhaa hafifu," alisema.
Alisema bidhaa zote zinazoingia nchini ziwe za biashara au misaada ni lazima zipimwe kwa lengo la kuondoa changamoto ya kuwauzia au kugawa zikiwa ni hafifu au kuisha muda wake.
Kwa upande wake, Ofisa Mdhibiti Ubora wa TBS, Salome Emmanuel alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuakikisha wanaingiza bidhaa zenye ubora na kuongeza wafanyabiashara ndio walinzi tosha wa kuhakikisha bidhaa hafifu haziingizwi nchini hivyo ni vizuri wakafuata sheria kukwepa tatizo hilo.
1 comment:
Mfanyabiashara waliomyanganya hizo diapers kaonewa. Whats next watatuambia tiolet paper nazo zinaisha muda wake ? Kakagueni madawa feki yanayouwa sio diapers
Post a Comment