ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 31, 2016

TRA: MADUKA YA KUBADILISHA FEDHA YATOE RISITI

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imezitaka taasisi zote za kubadilisha fedha kutoa risiti kwa wananchi wanapotoa fedha zao.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mamlaka hiyo kutambua kuwa inapoteza mapato mengi kutokana na taasisi hizo kutofuata utaratibu wa kutoa risiti wakati mteja anapokwenda kubadilisha fedha.
 Hayo aliyasema jana Dar es Salaam na Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Hamisi Lupenja katika semina iliyoandaliwa na TRA kwa wafanyabiashara, ikiwa ni muendelezo wa kutoa elimu ya kodi, matumizi ya mashine za kielektroniki EFDs na umuhimu wa kutoa risiti.
 “TRA baada ya kufanya uchunguzi dhidi ya wafanyabiashara hawa tukagundua tunapoteza mapato mengi sana kwani wengi wao hawatoi risiti pindi wanapotoa huduma kwa kisingizio cha mashine kuwa mbovu,” alisema Lupenja na kuongeza..
 “Pia tuliona ni vema kutoa elimu kuhusu kodi ya mapato na Kodi ya Ongezeko la Thamani VAT kwani wao ni walipa kodi lakini kuwapa ufahamu kwani wengine wao wanafanya biashara nyingine kubwa hivyo wanaweza kwenda kutoa elimu kwa wengine”.
 Hata hivyo Meneja wa Elimu, huduma kwa Mlipa Kodi TRA, Diana Masala alisema kuwa semina hiyo ni kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutoa risiti katika huduma zao wanazozifanya.
 “Kisheria ni kosa kutoa toa risiti katika huduma wanayofanya, hivyo tunataka wafahamu hilo pamoja na wananchi wanaokwenda kubadilisha fedha waombe risiti” alisema masala.
 Kwa upande wake Meneja Msaidizi Benki ya Tanzani (BOT), Omary Kacheuke alisema kuwa Disemba mwaka jana waliandaa semina ambayo ilihusisha wafanyabiashara hao na TRA ambapo yaliibuka malalamiko mengi.
 “Wafanyabishara hawa walilamikia kuhusiana na uharibikaji wa mara kwa mara wa mashine za EFD pamoja na usumbufu wa mtandao kila wakati kwahiyo tumeshukuru leo TRA imewaita wafanyabiashara hawa ili kuzungumza kuhusu matatizo hayo.
 Aidha liongeza kuwa mojawapo ya kero waliyokuwa wakiilalamika ni TRA kuwatoza kodi kubwa bila kuangalia kiasi cha mapato wanachoingiza katika biashara hiyo.
 “Kwa hiyo semIna hii itaweza kujibu maswali yote ambayo wafanyabishara hawa wamekuwa wakijiuliza lakini watapata elimu ya kodi na kuondoa kero zote”alifafanua.
 Mbali na hayo mmoja kati ya wafanya biashara hao kutoka ‘Cosat Bereau De Change’, Abdulbakari Abdalahm alisema hawana pingamizi na mashine za EFD kwani zinasaidia katika uandaaji sahihi wa taarifa za mapato.
 “Mfano zamani TRA wakija kuchukua kodi walikuwa wanatuchaji fedha nyingi sana tofauti na kiasi tunachoingiza kwani hakukuwa na mashine hivyo walikuwa wanaangalia kwa siku tumebadilisha fedha kiasi gani".
 Mfanyabiashaara huyo alisema matatizo yapo katika mashine hizo lakini si kwa kiwango kikubwa hivyo aliwataka wafanyabiashara wenzake kutumia pamoja na kutoa risiti wanapotoa huduma hizo.
CHANZO: NIPASHE

1 comment:

Anonymous said...

HAPO TRA MMEKULA BINGO MAANA WATANZANIA WOTE WALIKUWA WANAJIULIZA HIVI HAW MABWANA KWELI WANA LIPA KODI? MAANA WAONDIO WACHEZZA NA PESA TANGU ASUBUKH MPAKAUSIKU TENA FWEZA ZA KIGENI TU KWA SIKU KATIKA BIASHARA HIYO KUNA MZUNGUKO WA ZAIDI DOLLARS ZA KIMAREKANI ZAIDI YA MILLION 3 KWA SIKU ZA KAWAIDA HIVYO MKUSANYO WA KODI PEKE YAKE KWA JIJI LA DAR TU MNGEWEZA KOKUSANYA MPAKA DOLLARS LAKIMOJA AMBAZO SEREKALI INAZIKOSA KILA SIKU