Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kuadhimisha miaka 39 ya kuzaliwa
kwake na kumbukumbu hiyo itazinduliwa Januari 31,Unguja –Zanzibar chini ya mgeni
rasmi Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais
wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati
akitangaza maadhimisho ya chama hicho,Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa,Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema baada ya uzinduzi wa maadhimisho hayo Zanzibara,kilele chake kitakuwa mkoani Singida ambako zitafanyika kazi
mbalimbali ikiwemo na ya kuingiza wanachama wapya, kufanya kazi za kujiletea
maendeleo kwa kujenga madarasa,kupanda miti,pamoja na kufanya kazi za usafi .
Amesema viongozi wa kitaifa na baadhi
ya wajumbe wa Kamati Kuu watapangiwa shughuli za ujenzi wa chama na taifa kwa
ujumla katika wilaya za Mkoa wa Singida siku tatu kabla ya kilele ya
maadhimisho ambayo yatafanyika mkoani Singida.
Nape amesema mgeni rasmi katika
kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika Februari 6 mkoani Singida,anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa Chama hicho,Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Dk.Jakaya Kikwete.
Kauli Mbiu ya maadhimisho kwa Chama
hicho kwa mwaka huu kimetajwa kuwa ni “Sasa kazi,Kujenga Nchi na Kukijenga Chama”.Maadhimisho ya CCM hufanyika kila
Februari 5 ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa CCM Februari 5 ,1977 iliyotokana
kuungana kwa ASP na Tanu.
No comments:
Post a Comment