ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 30, 2016

UZIO WA HOTELI YA GOLDEN TULIP WABOMOLEWA LEO

Tingatinga likibomoa uzio wa eneo la maegesho ya magari wa hotel ya Hoteli ya Golden Tulip leo uliojengwa bila kufuata kibari halali.Picha na Othman Michuzi
Baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli ya Golden Tulip wakiendelea na zoezi la uondoshaji wa mabati yaliyoweka kama uzio katika eneo hilo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo hilo.

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

SERIKALI imevunja uzio wa eneo la maegesho ya magari wa hoteli ya  Golden Tulip Jijini Dar es Salaam kutokana na umiliki wa eneo hilo kutolewa kwa njia zisizo halali.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kushinda kesi dhidi ya Mmiliki wa mmiliki wa hoteli hiyo.

Kazi ya kubomoa uzio huo imefanywa kwa ushirikiano wa Baraza la Mazingira (NEMC, Manispaa ya Kinondoni pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumnba na Maendeleo ya Makazi kutokana na mmiliki huyo kushindwa kubomoa mwenyewe kwa maelekezo ya aliyopewa na Serikali.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la kubomoa uzio huo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa maeneo yote ya Ufukwe wa Bahari ni maeneo ya jamii hivyo hayatakiwi kuguswa kwa namna yeyote ile.

Waziri Lukuvi amesema serikali haitakubali kuona maeneo yanavamiwa na watu wachache kwa kuzunguka baadhi ya watendaji na kupata hati.

Amesema kuwa  katika kipindi hiki watafatilia maeneo yote ya ardhi kama yamevamiwa na yatarudishwa kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

Uzio wa Golden Tulip mara ya kwanza uliombwa kwa ajili ya kuegesha magari kwa muda katika mkutano wa SADC baada ya hapo mmiliki wa hoteli akaweza kupata hati ya eneo hilo kwa njia zisizo halali.

1 comment:

Anonymous said...

Malaika hotel in Mwanza watabomoa?