SIKILIZA MWENYEWE HAPA
“Joto la Bomobomoa” limezidi kuapanda kwa Wakazi wa Dar es Salaam hususani wale wanaotakiwa kubomoa nyumba zao zinazodaiwa kujengwa maeneo ambayo siyohalali.
Joto hilo limemkumba msanii maarufu wa Bongo Movies, Wastara Juma ambaye nyumba zake mbili hivi karibuni ziliwekewa alama ya X akitakiwa kuzibomoa.
Wastara aliyekuwa miongoni mwa mastaa kibao wa Bongo movies, Bongo Fleva na tasnia nyinginezo nchini alishiriki kwa kiasi kikubwa kupiga kampeni za uchaguzi wakati akikinadi Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika audio hapo chini, Wastara amefunguka mazito kuhusu nyumba zake kuwekwa alama ya “X” kwa ajili ya kubomolewa, huku akigusia kujitoa kwake kufanya kampeni ya kukinadi Chama Cha Mapinduzi kiasi cha kuugua.
3 comments:
mlitumwa mpigie debe CCM? Mtayaona sasa.
Ni hivi kwa vile umebomolewa wewe.Lakin ingekuwa haijakupata wala usingesikika humu mfyuuu.
Umesema ukibomolewa unaweza kukaa kwa magufuli sasa tatizo lako liko wapi na utwambie ni kivipi unaweza kwenda kukaa kwa Rais. Ni mjomba,shemeji au??
Post a Comment