ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 19, 2016

WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA BAADA YA KUKUTWA WAKIWA NA DAWA ZA KULEVYA

Madawa ya kulevya yaliyokamatwa mkoani Mbeya.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

“PRESS RELEASE” TAREHE 19.01.2016.
KATIKA TUKIO LA KWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NURU ISMAIL [31] MFANYABIASHARA NA MKAZI WA JIJINI DAR ES SALAAM ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI UZITO KILO 7 NA GRAMU 100 ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA KWENYE MABEGI YA NGUO.


MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.01.2016 MAJIRA YA SAA 05:30 ASUBUHI HUKO CUSTOM MPAKANI MWA TANZANIA NA ZAMBIA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

AIDHA MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA SAFARINI AKITOKEA SOUTH AFRIKA KUELEKEA JIJINI DSM AKIWA NA PASSPORT NO. AB.767234 ILIYOTOLEWA DSM TAREHE 21/10/2015 NA KUSAFIRI KWENYE BASI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.595 BPR MALI YA KAMPUNI YA FALCON IKITOKEA LUSAKA KUELEKEA DSM. 

KATIKA TUKIO LA PILI, MTU MMOJA MKAZI WA BITIMANYANGA WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA AITWAYE HAMIS SELEMANI [30] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 3 SAWA NA UZITO WA GRAMU 15 ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA MFUKONI MWA SURUALI YAKE.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.01.2016 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. 

WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA TU BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Imesainiwa na:
[EMANUEL G. LUKULA – ACP]

Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
NB: Kny – ina maana kwa niaba ya.

No comments: