ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 12, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU AAHIDI KULIKWAMUA JENGO LA ZAHANATI LILILOKWAMA SONGEA VIJIJINI

Hapa Kazi tu: Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni eneo la tukio alipotembelea ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mpingi mkoani Ruvuma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametembelea jengo la Zahanati ya Kijiji cha Mpingi wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo. 
Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazoendelea kuzifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mifuko ya afya.
Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na Halmashauri na wananchi, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiongozana na  Mkuu wa Wilaya ya Songea, Benson Mpesya waakati alipotembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo la Zahanati ya kijiji cha Mpingi, Mkoani Ruvuma leo.
Mzee Mohammed Mussa wa Kijiji cha Mpingi akimshukuru Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa kutembelea Kijiji hicho na kwa msaada wa mabati na misumari aliyowaahidi ili kumalizia ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho.
Baadhi ya Wanakijiji wa Mpingi waliohudhuria kumlaki Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipotembelea kijiji hicho.

No comments: