Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo
(katikakati) akimsikiliza Mbunge Mteule wa Jimbo la Ludewa, Deo Ngalawa (kulia) wakati wa ziara ya waziri
alipotembelea eneo la utafiti wa mradi wa
Makaa ya Mawe Mchuchuma.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo
akiongea jambo wakati akikagua sampuli
za Makaa ya Mawe wakati alipotembelea
Kampuni ya KATEWAKA Coal field, katika wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe.
Wengine ni ujumbe aliombatana nao na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mwenye Skafu ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Ludewa, Deo Ngalawa.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo akimsikiliza
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wilaya ya Ludewa, Raeuben
Sichone wakati waziri alipotembelea kituo cha Kufua umeme cha Mawengi, Ludewa k
wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya umeme mkoani Njombe.
Padre Jordan Mwanjonde wa
Parokia ya Lugalawa Jimbo la Mbeya, akimweleza jambo Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na ujumbe wake wakati waziri alipotembelea
mradi wa kuzalisha umeme unaomilikiwa na Jimbo hilo wakati wa ziara ya Waziri
utembelea miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Madaba wakizuia msafara wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo wakati akipita katika kijiji hicho kutoka Wilaya ya Ludewa kuelekea Mkoani Ruvuma, wakati wa ziara yake ya kikazi kutembelea miradi ya umeme na maeneo ya Utafiti wa Makaa ya Mawe Mkoani Njombe. Wananchi hao walimuomba Waziri awasaidie kupata nishati ya umeme katika kijiji hicho.
Diwani wa Kata ya Mdindi, Wilaya ya Ludewa, Waisi Mgine,
(wa pili kushoto mbele) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo (katikati) kuhusu ufafanuzi
wa ulipwaji wa fidia kwa wananchi
wa Kijiji cha Mdindi mara baada ya mradi wa Makaa ya Mawe utakapoanza baada ya
maeneo ya wananchi hao kuingizwa katika
eneo la mradi na mwekezaji Kampuni ya Tanzania International Resource Limited
kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo
ya Taifa (NDC).Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi.
Asteria Muhozya na Rhoda James - Njombe
Serikali imesema matarajio yake ni kuona kuwa
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linajiendesha kibiashara kuhakikisha kuwa
wazalishaji wanaliuzia shirika hilo umeme kwa bei ambayo haitawaumiza
wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo (Januari 11,) na Waziri
wa Nishati na Madin, Profesa Sospeter Muhongo alipotembelea eneo la
utafiti la Makaa ya Mawe Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe.
Profesa Muhongo alieleza kuwa, endapo Tanesco
itanunua umeme kwa bei ya juu kutoka kwa wauzaji inamaanisha kuwa
itaendelea kuwauzia wananchi umeme wa bei ya juu ambapo pia Serikali
italazimika kutoa ruzuku kwa shirika hilo ili lijiendeshe.
"Tunatoka huko sasa. Hatutaki tena kuendelea
kuwapa Tanesco ruzuku, tunataka shirika hili lijiendeshe kibiashara lakini pia
hatutaki kuwaumiza wananchi."
Kauli ya Waziri Muhongo imekuja kufuatia
kutokukubaliana kwa gharama za kuuziana umeme mara baada ya mradi wa Makaa ya
Mawe ya Mchuchuma utakapoanza kuzalisha umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe,
ambapo Kampuni ya Tanzania International Resource Limited ambayo ni
mbia wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) katika mradi wa Makaa ya Mawe
kupanga kuiuzia Tanesco umeme kwa bei ya kiasi cha senti za Marekeni 13
ambapo Tanesco wanataka kununua kwa nusu ya bei hiyo.
Kufuatia hali hiyo Profesa Muhongo aliitaka kampuni
hiyo ya NDC na TANESCO kukaa kikao chini ya Uenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana
Pallangyo siku ya Jumatano, Januari 13, 2016 ili kujadiliana kuhusu suala hilo
na kufahamu mustakabali wa uendelezaji wa mradi huo ambao utakapokamilika,
unatarajiwa kuwezesha uzalishaji wa megawati 600 za umeme ambazo kati yake
megawati 350 zitaingizwa katika Gridi ya Taifa.
"Tunataka mradi uiuzie Tanesco umeme kwa bei
rahisi lakini pia tufike mwisho wa majadiliano na mradi uanze haraka. Endapo
hatutaafikiana katika hili tutafute mwekezaji mwingine," alisema Profesa
Muhongo.
Akizungumzia kuhusu suala la fidia kwa wananchi
waliopisha mradi huo, Profesa ameitaka kampuni hiyo kuharakisha suala la fidia
na kuwaruhusu wakulima kutumia ardhi kwa shughuli za kilimo cha mazao ya
muda mfupi wakati makubaliano kati ya Tanesco na kampuni yanaendelea.
Naye Mbunge Mteule wa Jimbo la Ludewa Deo Ngalawa
amemshukuru Profesa Muhongo kwa kufika kwake na kuendesha majadiliano kuhusu
mradi huo na kuongeza kuwa, jitihada za Profesa Muhongo katika kuongeza kiwango
cha umeme nchini zinaonekana na kwamba wananchi wa Ludewa wanausubiri mradi huo
kwa kuwa ni ajira na fursa kwao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Antony
Choya amemuelezea Profesa Muhongo kuwa amekuwa ni zaidi ya Mwalimu katika
kuwafahamisha kuhusu mradi huo na namna anavyosimamia masuala ya nishati na
hususan kutafuta ufumbuzi juu ya mradi husika.
No comments:
Post a Comment