Advertisements

Tuesday, February 9, 2016

BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA CHAN, WACHEZAJI WA DR CONGO WAZAWADIWA MAGARI YA KIFAHARI



Goli mbili kutoka kwa Meshack Elia pamoja na goli moja kutoka kwa Jonathan Bolingiyalitosha kuwapa ubingwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye michuano iliyofanyika Kigali, Rwanda mwaka 2016.
Congo DR iliitoa Rwanda ‘The Amavubi’ kwenye robo fainali kwa kuitungua bao 2-1 kwenye dakika za nyongeza kabla ya kushinda kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya Guinea kwenye mchezo wa nusu fainali.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Congo DR kila mmoja amepewa zawadi ya gari la kifari baada ya kufanikiwa kushinda kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani CHAN walipoifunga Mali kwa bao 3-0 kwenye mchezo wa fainali.
Kwa mujibu wa BBC online, Rais Joseph Kabila amempatia kila mchezaji aliyekuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa gari la kutembelea aina ya Prado lenye thamani ya dola za kimarekani 60,000.

3 comments:

Anonymous said...

Amekosa pesa ya uchaguzi, anajaribu kuandaa njia ya kungangania madaraka.

Anonymous said...

Akili ya Muafrica unaacha kuwapa nyumba au viwanja vya kujenga unawapa magari? wataishi ndani ya gari?

Anonymous said...

Yaani Congo na matatizo yote. Miundo mbinu, huduma za jamii, umasikini uliotopea, eliminerer,afya, kote huko, hawa viongozi wao vihio hawazioni bali kwenye starehe tu,Hili bara linangushwa na vingozi wasio jua Nini? Maana ya uongozi. Ni shidaa,