Meneja Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua vyoo vyenye matundu 14, vitakavyohudumia wanafunzi 850 katika shule ya Msingi ya Makambi, Songea Mkoa wa Ruvuma, ujenzi huo umegharimu shilingi milioni 4.7 kulia ni Meneja wa Oparesheni wa tawi la Songea, Simon Mlelwa.
Meneja Mwandamizi wa
Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akiongea kwenye mkutano katika shule hiyo muda mfupi kabla ya kuzindua vyoo hivyo.
Meneja
Mwandamizi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta, Noves Moses akiwa
kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule hiyo pamoja na baadhi ya viongozi wa
serikali ya mtaa.
|
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Makambi iliyopo Kata ya Ndilima Litembo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifurahia vyoo vya kisasa vilivyojengwa na Benki ya Posta Tanzania.
Na Mwandishi Wetu
MENEJA mahusiano na
mawasiliano wa Benki Posta Tanzania, Noves
Moses amelitaka suala la elimu bure liendane na mazingira mazuri ya kimiundo
mbinu kwa wanafunzi pamoja na walimu wao ili kuifanya elimu hiyo kuwa bora
zaidi.
Rai hiyo aliitoa
jana wakati akizindua vyoo vya kisasa vya Shule ya Msingi ya Makambi iliyopo Kata ya Ndilima Litembo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, ambavyo vimejengwa na
Benki hiyo kwa thamani ya shilingi Milioni 4.7 ikiwa ni sehemu
ya mchango kwa jamii katika kuboresha mazingira ya elimu.
Akizindua matumizi
ya vyoo hivyo vyenye matundu 14, Noves alisema kuwa
jamii na taasisi mbalimbali zinatakiwa zitambue kuwa suala la elimu bure
linatakiwa liendane na uboreshwaji wa mazingira ya
wanafunzi na walimu wawapo shuleni hapo.
Alisema kuwa kumekuwepo
na baadhi ya wadau wa elimu kulichukulia suala la elimu bure kama kigezo cha kutokuchangia sekta hiyo na baadala yake
wanadai ni kazi ya serikali pekee jambo ambalo siyo sahihi katika uboreshaji
elimu.
“Suala la elimu bure
lisiwe kigezo cha wadau kushindwa kuichangia sekta hiyo kwani kufanya hivyo
kunapelekea baadhi ya shule kushindwa kuwa na mazingira mazuri ya watoto
kujisomea pamoja na walimu wao kutokuwa na morali ya kufundisha” alisema
Meneja mahusiano .
Noves alisema kuwa
Benki ya Posta Tanzania inafanya kazi kwa kiwango kikubwa na serikali
hivyo imetoa misaada mbalimbali ya kijamii hasa kwa upande wa afya na elimu
huku katika upande wa elimu wamechangia madawati na ujenzi wa vyoo bora vya
kisasa kwenye shule mbalimbali hapa nchini .
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi wa
shule hiyo, Kanisius Ngongi awali akitoa taarifa ya shule hiyo kabla
ya kukabidhiwa vyoo hivyo alisema kuwa shule hiyo ina wanafunzi
850 na matundu ya vyoo yapo 14 na kuwa vyoo vyote vina maji
ya kutosha.
Ngongi aliipongeza benki hiyo alisema kuwa shule hiyo kwa sasa
imeshabadilika, mazingira yamekuwa bora kwa upande wa vyoo vya wanafunzi
ambavyo kwa sasa hakuna shule ndani ya Manispaa hiyo yenye vyoo kama hivyo.
Mwalimu Ngongi
alisema kuwa licha ya vyoo vya wanafunzi kuwa bora lakini bado kuna changamoto
ya vyoo vya walimu maana vyoo walivyokuwa wakivitumia vimeshapoteza ubora wake
na kuwafanya walimu hao kupata shida mahala pa kujisitili hivyo amewaomba wadau
mbalimbali waweze kuchangia kama Benki ya Posta
inavyojitolea.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment