Meneja wa Mradi wa kitengo cha haki Jinsia kutoka Oxfam Bi. Rishida shariff akielezea kwa kina namna walivyofanya mradi wa Fahamu Ongea Sikilizwa
Mtafiti mkuu wa kuhusiana na ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 Profesa Ruth Meena akifafanua kwa kina namna ya utafiti ulivyofanyika.
Dkt. Alexander Makulilo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam akifanya uchambuzi wa namna utafiti ulivyofanyika.
Aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu Mwaka 2015 Mama Anna Mgwila akichangia jambo wakati wa uzinduzi huo
Baadhi ya wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Idara ya Uratibu Shuguli za SMZ Dar es salaam wa kwanza na wa pili (Kushoto) na Bi. Msangu Said (wa tatu kushoto) kutoka shirika la utangazaji la Zanzibar ZBC
Baadhi ya wadau waliohudhulia katika uzinduzi wa Ripoti ya ushiriki wa wanawake katika uchaguzi mkuu 2015
Baadhi ya vijarida na Ripoti
(Picha na Fredy Njeje Blogs za Mikoa)
(Picha na Fredy Njeje Blogs za Mikoa)
Kitengo cha Haki
za jinsia cha Oxfam nchini Tanzania Fahamu Ongea Sikilizwa(FOS) imezindua
kitabu chake cha utafiti kughusu taarifa za kushiriki kwa wanawake kati masuala
ya uchaguzi mkuu maka 2015 na 2016 nchini Tanzania.
Uzinduzi wa
taarifa hiyo umefanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Double view na Meneja wa kitengo cha haki
za binadamu na jinsia kutoka Oxfam Bi. Rashida Shariff huku akieleza baadhi ya
mikoa iliyofanyiwa utafiti huo kuwaTanzania bara kwa mikoa nane ikiwemo
Shinyanga, Dodoma, Tanga, Arusha, Dar es
salaam, Morogoro,Lindi na Mwanza na Tanzania visiwani Zanzibar ni Kusini Unguja
Bi. Rashida
amebainisha lengo kuu la utafiti huo likiwa ni kuwapauwezo wa kujiamini wanawake
kushiriki kikamilifu katika kujitokez kikamilifu kupiga kura pamoja na kujikita
kwenye masuala ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini bila woga.
Aidha
ameongeza kuwa utafiti umelenga kupata changamoto za wanawake walizokuwa
wanapata hususani kwa wagombea ambapo wagombea sita wanawake kutoka katika
vyamba mbalimbali vya siasa Mh. Angelina Mabula, Anna Mghwira, Nancy Mrikaria,
Khadija Msawira, Magreth Mshenene na Mh. Safia Mkamama wametumiwa kuelezea
changamoto zilizowakabili na mafanikio waliyoyapata ikiwemo ni pamoja na
kuongeza kujiamini
Kwa upande
wake aliyekuwa mgombea urais kwa kupitia Chama cha ACT -Wazalendo Anna Ngwila
amesema kuwa ushiriki wa wanawake katika uchaguzi bado umeelekezwa kwenye
ushabiki ambapo wanawake hutumiwa katika vyama kwa lengo la kutoa kura zao
kuliko wao wenyewe kugombea.
Bi Anna
akitolea mfano yeye mwenyewe alisema kuwa changamoto aliyokumbana nayo ni ndani
ya vyama ilikuwa ni kutiliwa mashaka kama ataweza mikikimikiki ya uchaguzi
lakini wanasahau kuwa wanawake nao wanaweza kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili kijamii.
Naye mtafiti
mkuu wa utafiti huo Profesa Luth Meena ameongezea
kuwa taarifa hii itasaidia vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo vyama vya
siasa, msajili wa vyama vya siasa, tume za uchaguzi, vyombo vya habari,
TAKUKURU, pamioja na Asasi za kiraia na jamii kwa ujumla kuzumgumzia kwa
usahihi ikiwemo kuchukua hatua za kisera, kisheria katika kuleta usawa wa
kijinsia katika michakato ya uchaguzi huku ikiwapa uwezo wa kujiamini kwa
wanawake katika kushiriki katika masuala ya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment