Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua
mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa. Katibu huyo
mkuu wa Fifa alipata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya
mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne
huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja. Tokyo
Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.
Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum'baini mshindi wa
moja kwa moja. vWingi
wowote wa kura (zaidi ya aslimia 50) katika raundi ya pili ya uchaguzi huo
ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig
jimbo la Valais nchini Switzerland, ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita
kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter
ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita
kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha
miaka sita .
Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe
waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo. Lakini
aliwaambia wajumbe kwamba ''kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na
heshima ya Fifa''.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment