ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 16, 2016

Habari Mbaya:Rapper John Woka Afariki Dunia Baada ya Kupata Ajali ya Kulipukiwa na Gesi


Rapper anayejulikana kwa kurap kama mlevi, Michael Dennis Mhina maarufu kama John Woka, amefariki dunia alfajiri ya Jumanne hii.

Woka amefariki baada ya juzi kupata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Hii ni taarifa iliyotolewa na mtu wa karibu na rapper huyo kuelezea ajali hiyo:

Walikuwa wanahangaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka,moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.

Kwa yeyote aliyeguswa na angependa kutoa rambi rambi anaweza kuwasiliana na kaka yake kwa namba +255767007005.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

No comments: