Idris Sultan na mpenzi wake Wema Sepetu wanakuja na reality TV show ambayo itakuwa inazungumzia maisha yao.
Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Idris alisema ameamua kuungana na mpenzi wake Wema ili kuandaa project mbalimbali ambazo zitakuwa zinawaingizia pesa.
“Unajua mkiwa katika mahusiano halafu wote ni celebrity lazima angalau mfanye kazi mbili tatu ambazo zitawaingizia pesa,” alisema Idris.
“Zipo project nyingi lakini tunaanza na reality show. Hii ni nyingine na mpya na itakuwa inazungumzia matukio mbalimbali ya maisha yetu,” aliongeza Idris
Source:Bongo5
2 comments:
Naingoja kwa hamu nichanell gain SAA ngapi nalini ?
Ninyi nao. Biashara zoote duniani kujionyesha maisha yenu ndio biashara kubwa mlioifikiria kufanya!!.... Ok. Good luck!
Post a Comment