ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 16, 2016

Hatimaye Rommy (DJ wa Diamond) Arejea Kazini Baada ya Kusemekana Wametofautiana na Diamond Platnumz


Sina uhakika kama Diamond na Rommy waligombana lakini kwa habari za chini chini inasemekana kuwa Rommy na Diamond walitofautiana ingawa wao hawakuthibitisha hilo!
Taarifa za chini chini zinasema kuwa Rommy na Diamond walitofautiana baada ya Rommy kuambiwa ajitegemee! Ndipo Rommy alipo kaa mbali na WCB na kuamua kuanza kurusha Matangazo katika Ukurasa wake wa Insta! matangazo yalio kuwa yana muhusu diamond alikuwa anatoa kwa kuibia ibia sana

Ikumbukwe kuwa show za Diamond zote Rommy alikuwa ndio Dj lakini baada ya kutofautiana kwao hakuonekana tena kwenye show hadi Usiku wa Mkesha wa Valentines day ambapo Diamond Alifanya Show kubwa Kisumu Kenya

Wakiwa na Crew ya WCB kenya Rommy ameonekana kwenye picha ya pamoja jambo ambalo watu wamesema ni kutokana na kumaliza tofauti zao na hivyo ataendelea kuwa Dj wa Diamond katika show zake zote

Juzi Rommy alipost videos mbili zikionesha akiwa kwenye Ndege kuelekea kenya ingawa yeye hakusema kama anaende kenya ndipo Esmaplatnumz alipo comment na kusema nakuona Rommy Nairobi Moja!

Diamond nae alipost video akionesha anatoka SA kwenda Kenya kwenye show!

Ule usemi wa kuwa Ndugu wakigombana Shika Jembe ukalime ni dhahiri kuwa umetimia!

Sasa Diamond + Rommy wapo pamoja tena na Kazi zinaendelea! kama ni kweli waligombana Hongera kwa alie wapatanisha!

No comments: