ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 15, 2016

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AZINDUA BODI YA CHUO CHA UHAMIAJI CHA KIKANDA (TRITA) MJINI MOSHI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi. Katika hotuba yake Rwegasira aliitaka Bodi hiyo ifanye kazi kwa ushirikiano kwa maendeleo ya chuo. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Kinemo Kihomano. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika mjini Moshi. Watatu kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Kushoto ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Kinemo Kihomano.na kulia ni Kamishna wa Chuo hicho, John Choma.
Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Erasmi Francis akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) na wajumbe wa Bodi ya Chuo hicho, kamera inayotumika kuchukua kumbukumbu za usalama kwa ajili ya watu wanaopita katika mipaka ya nchi. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Watatu kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Kinemo Kihomano (Wasita kushoto).
 Mkaguzi wa Uhamiaji ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Zawad Chazuka akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati) albamu yenye hati za kusafiria za mataifa mbalimbali duniani, albamu hiyo inaonyesha alama za kiusalama ambazo zipo katika pasipoti za mataifa mbalimbali. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi, Kinemo Kihomano, akizungumza na wajumbe wa bodi (hawapo pichani, mara baada ya bodi hiyo kuzinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati). Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli, wakati alipokuwa anawasili katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi kwa ajili ya kuzindua Bodi ya Chuo hicho
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akikagua maeneo mbalimbali ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) mjini Moshi. (kushoto) mara baada ya kuzindua Bodi ya Chuo hicho. Katikati ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli, na kulia ni Kamishna wa Chuo hicho, John Choma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati waliokaa), Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), mara baada ya Katibu Mkuu huyo kuzindua Bodi hiyo mjini Moshi.

No comments: