ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 15, 2016

UTENDAJI: Mrema, Rungwe wamchambua JPM

By Elizabeth Edward, Mwananchi; eedward@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema amesema hajutii kumpigia debe Rais John Magufuli wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Pamoja na kutoswa ubunge, alidai jana kuwa bado anasimamia ukweli kwamba Rais Magufuli ndiye mtu aliyestahili kuliongoza Taifa hili.

Wakati Mrema akisema hayo, Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe amewataka Watanzania kuacha kummiminia sifa Rais Magufuli kwa kile alichoeleza kuwa ni wajibu wake akiwa kiongozi mkuu wa nchi.

Mrema

Akizungumza na gazeti hili, Mrema alisema kumnadi Magufuli kwa wananchi wa Vunjo kulitafsiriwa vibaya na ndiyo sababu waliamuadhibu kwa kumpiga chini katika kinyang’anyiro cha ubunge.

“Nilijua wazi Rais Magufuli ni mtendaji ndiyo maana hata wananchi waliponiadhibu kwa sababu ya kumpigia debe sikuumia, najivunia chaguo langu na kiukweli anafanya miujiza ya hali ya juu.

“Kumpata kiongozi mwenye uthubutu kama alionao Rais Magufuli ni kazi kubwa Watanzania tuache unafiki tumpe nafasi afanye mambo makubwa zaidi,” alisema Mrema.

Hashim Rungwe

Alisema haoni kama kuna kitu kikubwa ambacho Rais Magufuli amekifanya tangu aingie madarakani zaidi ya kuendeleza kazi walizofanya wengine.

Alisema kumwagia sifa kupita kiasi ni ishara kwamba viongozi waliotangulia hawakuleta maendeleo jambo ambalo alidai halina ukweli.

Akitolea mfano sera ya elimu bure alisema utekelezaji wake usingewezekana kama Rais wa awamu iliyopita (Jakaya Kikwete) asingewekeza kwenye ujenzi wa shule za kata. “Unaweka elimu bure wakati watoto bado wanashinda njaa, unategemea wanachofundishwa wataelewa kweli kama siyo kupoteza muda basi atoe na chakula,” alisema Rungwe aliyeshiriki kinyang’anyiro cha urais mwaka jana.

1 comment:

Anonymous said...

Huyu mzee Rungwe anazungumza kitu gani? Kama si hofu ya kushutumiwa na wanablogu yakuwa natumia lugha isiifaa nathubutu kusema huyu mzee anazungumza utumbo wa aina gani? Raisi asipongezwe kwa kazi nzuri anaoifanya kwa kuwa ni wajibu wake kama kiongozi mkuu wa nchi? Basi na raisi itakapotokezea serikali yake kufanya madudu watu wafumbe midomo yao wanyamaze kimya. Eti haoni kitu kikubwa muheshimiwa raisi alichokifanya tangu raisi aingie madarakani? Huyu mzee anaakili kweli na macho na masikio yaliotimamu? Kodi ya mwezi inayokusanywaa na serikali ya Magufuli ilikuwa inakusanywa kwa miezi sita na serikali ya kikwete. Halafu tunaambiwa huyu mzee alikuwa anagombea uraisi? Ama kweli kazi ya uraisi ilizaraulika sana Tanzania. Huyu mzee anakwenda mbali zaidi kukejeli dhamira nzuri ya muheshimiwa raisi ya kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania mwenye umri wa kwenda shule anakwenda shule na anapata elimu bure. Kila kitu kinachoanzishwa kina changamoto zake na moja ya changamoto kubwa ni kutokezea kwa watu wapuuzi watakaobeza ile zamira nzuri kwa kutoa maneno ya kukatisha tamaa baada ya kutoa mawazo ya manufaa yatakayosaidia kuboresha malengo yaliokusudiwa. Kama tatizo ni njaa kwa wanafunzi basi ni wakati wa kufanya jitihada kuwapatia wanafunzi chakula baada ya kwenda kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya dharau ingekuwa busara kutumia huo wasaa kutoa wito kwa watanzania wenye uwezo kuanzisha na kuchangia mfuko wa chakula cha wanafunzi mashuleni.Tanzania sio ya magufuli peke yake na magufuli sio mwendawazimu wala hafanyi anayoyafanya kwa kutaka sifa. Magufuli ni miongini mwa wazalendo wachache wa kweli kuwahi kutokea katika taifa lolote duniani sio Tanzania tu. Hata hizo nchi za Magharibi zimesita kipindi kirefu kuzalisha watu wa aina za kina magufuli. Labda tunaweza kusema yakwamba zile tabiri za miaka mingi yakwamba ipo siku Africa itamka nakuwa bara lenye uchumi zaidi duniani wakati wake umewadia kwa mungu hakuna kubwa kwa Mungu kuwaleta viongozi wenye nguvu iliotukuka ya uwajibikaji wa kiwango cha Magufuli si bure kuna jambo kubwa linakuja Africa.Africa tatizo moja kubwa linalotafuna ni ukosefu wa viongozi waadilifu. Na watanzania tutakuwa watu wa ajabu sana kama tutakaa pembeni kumuachia magufuli peke yake atujengee nchi yetu sote. Magufuli ni kiongozi wa kupigiwa mfano kabisa hata anavyoongoza serikali yake huwezi kusema kawekwa pale na chama fulani. Kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani amekuwa mtumishi wa umma zaidi bila ya kujali tofauti ya wale anaowatumikia. Amekuwa akikemea uozo bila ya kigugumizi cha aina yeyote amekuwa akiikosoa serikali ya CCM kwa kushindwa kutimiza majukumu yake chini ya uongozi wa kikwete hadharani. Ni kiongozi mwenye dhamira ya kuleta maendeleo ya kweli Tanzania. Na kama watanzania watampa muheshimiwa raisi ushirikiano wa kweli basi kipindi kifupi kijacho watu wataisoma namba Tanzania. Kama muheshimiwa raisi anavyosema Tanzania ni tajiri na ni kweli kuanzia hali ya hewa mpaka udingo ni utajiri mtupu kutokujitambua kwetu ndiko kunakotufanya kushindwa kuthamini na kuvitukuza vya kwetu mtu anajisifia yeye ni mmerekani wakati ndugu zetu wadhalia weusi wa hapa utambulisho wao ni African American wengine ni wazungu weupe kabisa. Kwetu sisi mtanzania halisi anarangi kidogo yeye mwarabu lol,hadi unataka kutapika nadhani ipo siku tutaondokewa na upumbavu wetu kwani watanzania ni miongini mwa waafrica wa hovyo huku nje wanaojifanya wamestaarabika kwa kudharau walipotoka bila ya kujua watu wanawacheka kwa upuuzi wao.