ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 11, 2016

KPMG yawa kinara kundi lao katika michuano ya Awesome Bonanza 2016

Kikosi cha timu ya KPMG  Waliosimama kutoka kushoto ni Isyaka,Bakari,Isaya, Nsanyiwa,Hamza(kocha),Getrude(kiongozi wa timu) na Jovin.  Walioinama kutoka kushoto ni  Evans, Denis, Jamal, Thobias, Frank, Ahmed na Amiri.    Aliyelala ni Jim aka Messi wa KPMG katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine
 Kikosi cha wachezaji wa Kampuni ya KPMG katika picha ya pamoja katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine
 Wachezaji wa timu ya KPMG wakiwa mapumziko kutoka kushoto walioangalia mbele Bakari , Dennis, hamza (kocha mchezaji) na isyaka katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine
Wachezaji wa timu ya KPMG wakishangilia Goli dhidi ya Timu ya Deloitte katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine
Wachezaji wa KPMG wakishangilia Goli lilifungwa na mshambuliaji wao machachari Daudi Mbaga dhidi ya  timu ya PWC katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine
 Kiungo wa Timu ya KPMG Bakari Mkupe akiwania mpira na wachezaji wa Timu ya PWC.katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita ambapo michuano hiyo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine
Wafanyakazi  wa kampuni ya KPMG waliokuja kushangilia wenzao  kutoka kushoto ni Asha, Mumtaz,Lilian, Witness, Getrude, patricia, desire na Grace.katika michuano ya Awesome Bonanza mwishoni wa wiki iliyopita imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine



Na Krantz Mwantepele,Dar es salaam                                                                                              

Timu ya mpira wa miguu ya kampuni ya uhasibu ya KPMG ilishiriki michuano ya Awesome Bonanza siku ya Jumamosi tarehe 6-Feb 2016 na kuibuka kinara katika kundi lao lililohusisha timu nyingine za makampuni yanayohusika na uhasibu pia.
 Michuano hiyo ambayo imeandaliwa na Jarida la kila mwezi la Awesome magazine ilianza siku ya jumamosi tarehe 6 feb 2016 ikifanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Park vilivyopo maeneo ya Mnazi Mmoja zamani kidongo chekundu kwa hatua za Makundi kwa kundi la timu kutoka kampuni  za uhasibu.

Katika kundi hilo zilikuwepo timu kutoka kampuni za uhasibu za Deloitte, PWC na Innovex.
Timu ya kampuni ya  KPMG iliibuka kinara wa kundi hilo kwa kupata ushindi katika mechi zao zote. KPMG ilipata matokeo yafuatayo: KPMG 3-1 PWC, KPMG 4-1 Deloitte , KPMG 2-1 Innovex. Hivyo kuwafanya wasonge mbele katika micuano hiyo itakayoendelea mwezi huu.
Wafungaji wa magoli ya KPMG walikuwa
Jim Mwasigala (3)
Bakari Mkupe (2)
Frank Mboya (2)
Ahmed Mohammed
Daudi Mbaga
Akiongea baada ya mechi hizo kocha mchezaji wa timu ya KPMG, Hamza Mzee amesema ya kwamba timu kampuni ya KPMG imejiandaa vyema na wana uhakika wa kushinda michuano hiyo kwa kuwa wanajali utamaduni wa kufanya mazoezi kupitia michezo kwa kuwa huboresha Afya kwa ujumla.




No comments: