Maalim Seif anasisitiza kwamba uchaguzi ulishafanyika na kukamilika tarehe 25 Oktoba, 2015 na umethibitishwa na waangalizi wote kuwa ulikuwa uchaguzi huru na wa haki. Waangalizi hao ni pamoja na wale wa Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na waangalizi kutoka nchi za Marekani na Uingereza.
Anasema kwamba kitendo cha kupindua maamuzi ya Wazanzibari kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kilifanywa kwa baraka zote za aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati huo, Jakaya Kikwete. Anasema hakuna mtu mbaya kwa Zanzibar na Wazanzibari kama Jakaya Kikwete. Kwa hivyo, anasema kudai kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano hana mamlaka kuliingilia kati suala la Zanzibar ni unafiki wa hali ya juu.
Maalim Seif ameweka msimamo wa CUF hadharani kwamba uchaguzi wa marudio si halali na si ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi uliopo huku akisisitiza kwamba uchaguzi ulishafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.
Amewaeleza kwa kina yaliyojiri katika vikao 9 vya mazungumzo kati yake na Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Marais wastaafu na kuweka wazi kwamba mazungumzo hayo hayakufanikiwa kwa sababu Dk. Shein hana nia njema na si mkweli. Amesema Dk. Shein ni mtu anayeamini kutawala kwa mabavu na matumizi ya nguvu na asiyejali wala kuheshimu Katiba.
Maalim Seif anawataka wana-CUF kutembea kifua mbele wakijua kwamba wao ndiyo WASHINDI HALALI wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
Amemalizia kwa kusisitiza tena kwamba msimamo wa CUF kama ulivyotangazwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa UKO PALE PALE!
2 comments:
Alaniwe kikwete Na Magufuli
Nani kwa kuambia wee mtoto waweza kulaani baba yako au mama....wendawazimu huo tuliza boli mutu weye....shuwaini...
Post a Comment