Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika hapo kesho na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuelekea Ikulu jijini Dar es salaam kushinikiza kurejeshwa ka matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Naibu Kamishna wa Polisi Simon Siro amesema Chama hicho kinatakiwa kutumia mbinu nyigine ya kushinikiza kurejeshwa kwa matangazo hayo ya Televisheni ya Taifa na sio kupitia maandano.
Katika hatua nyingine jeshi hilo limesitisha kazi za vikundi vya ulinzi shirikishi katika kituo cha kati kutokana na kufanyika kwa vitendo vyenye harufu ya rushwa, kutofuata sheria za ukamataji pamoja na kutumia nguvu kupita kiasi huku Naibu Kamishna Siro akianisha kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kukamata wanaokiuka taratibu.
7 comments:
Maandamano ni haki ya msingi kwa raia taifa letu linaogopa maandamano kama ukoma,bado tunatawaliwa na mawazo ya kale ya siasa za chama kimoja.
Polisi kazi yenu nini? kulinda usalama wa raia na mali zao sasa kama mmechoka kazi semeni sio kuzuwia maandamano hiyo sio kazi yenu,mnachotakiwa kufanya ni kuweka ulinzi na maandamano yafanyike kwa usalama bila mtu kudhurika huu imekuwa mchezo katika taifa letu, woga wa viongozi na serekali yake ndio imekuwa kigezo cha kuwakosesha wananchi haki zao za msingi.
mdau.
Iringa.
HUKU NI KUDHIHIRISHA WAZI HOFU UWOGA NA WASI WASI WA KUTOJIAMINI WANACHOKIFANYA, TAIFA LILILO HURU NA LENYE VIONGOZI MAKINI NI WALE WENYE KUJIAMINI NA KUKUBALI KUKOSOLEWA, HII NI DHAHIRI WANACHOKIFANYA JUU YA WANANCHI SI SAHIHI WANAJARIBU KUFICHA MAKUCHA YAO, KUKOSEA NA KUKOSOLEWA NDIO UUNGWANA, TUJENGE TAIFA LA UDIKTEKTA
Chadema hama busara..badala ya kuwaongoza watu wenu kwenye shughuli za kimaendeleo na ujenzi wa nchi, mnapoteza muda kuandamana? Kwa sababu Rais amesimamisha kurushwa Televisheni bungeni ili kuokoa fedha? Watanzania tuamke jamani, na tutumie akili kuliko mambo ya kitoto kama haya. Nyie upinzani mnatuabisha sana kwani kila suala, hata la kipumbavu kama hili, mnasema hamna "demokrasi" blaah blaah blaah...mnakariri kama watoto wa shule za msingi! Kama hawa waandamanaji hawana kazi/ajira, basi wanaweza kulisaidia jiji la Dar kwa kujitolea kufanya usafi kwenye mitaa au mazingira wanayoishi, kitendo ambacho ni cha kiungwana na cha KIDEMOKRASIA!
Katika shida na matatizo yanaowakabil watu kila siku cdma wameona matangazo ya bunge live ndio muhimu? Wakati hata marekani cspan kuangalia congress live sio bure lazima ulipie cable. Nawaunga mkono tbc 100% hizo billioni wanazotumia kurusha matangazo live zitumike kuboresha station yao. Bunge lenyewe badala kujadili sera na shughuli za maendeleo ni kusutana na nani katoa mpasho wa siku
Wanaficha nini bungeni bwana!?
Wanaficha nini bungeni bwana!? Kwani matumiziya kurusha hewani bunge pekee ndiyo yanamalipa peaa za nchi? Amka basi
Kwa namna ambayo bunge limekosa mwelekeo na kugeuzwa kijiwe cha mipasho hata hiyo recorded program wangeondoa wakatuwekea vipindi vya comedy.
Post a Comment