ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 16, 2016

MAGHEMBE APONGEZA JUHUDI ZA KURUDISHA MBWA MWITU SERENGETI.

MAG1 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (MB) akisalimiana na Mhifadhi Ashery Loishooki mara baada ya kuwasili katika eneo la Nyasirori, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita katika boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
MAG2Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) katika tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
MAG3
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akiongeawakati wa tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
MAG4
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akielekea katika boma la mbwa mwitu kwa ajili ya tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
MAG5
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akikata utepe kuruhusu kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kutoka nje kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
MAG6Wanahabari wakichukua picha mbalimbali wakati mbwa mwitu walipokuwa wakitoka kwenye boma.
MAG7
Kundi la sita la mbwa mwitu 11 wakitoka katika boma maalum katika Hifadhi ya Serengeti.
MAG9Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi akiongea na wanahabari mara baada ya tukio la kuachiwa kwa mbwa mwitu.
MAG11

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (MB) akiwa katika picha ya pamoja na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 



Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amepongeza jitihada zinazofanywa na watafiti kwa kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Taifa Serengeti baada ya kutoweka katika miaka ya tisini. Waziri Maghembe alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipokuwa akiachia huru kundi la sita la mbwa 17 waliokuwa wamehifadhiwa katika boma maalum ili kurejea katika makazi yao ya asili. 


Profesa Maghembe amesema serikali itaendelea kuwekeza katika eneo la utafiti ili kuwezesha sekta ya uhifadhi nchini kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa. Alisema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sekta nyingi ikiwemo ya uhifadhi na kuwa wanyama wamekuwa wakiathirika na mabadiliko hayo hivyo ni vema uwekezaji mkubwa ukafanyika katika eneo la utafiti ili kujua namna ambavyo uhifadhi unaweza kukabiliana na mabadiliko hayo. 

Mradi wa uhifadhi wa mbwa mwitu unalenga kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambao walitoweka kabisa tangu mwaka 1994 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaweza kubainika kisayansi. Mradi huu unasimamiwa na kuendeshwa na watafiti wa kitanzania. 

Tangu kuanza kwa mradi huu mwaka 2011, jumla ya makundi sita ya mbwa mwitu wamesharudishwa ndani ya Hifadhi ya Serengeti. Makundi haya ni pamoja na Vodacom ambapo Kampuni hii ya simu ilifadhili gharama za mradi; Serengeti; Loliondo; Kikwete; Nyasirori na hili la mwisho ambalo lilipewa jina la Markus Borner, mwanasayansi kutoka nchini Ujerumani aliyetumia miaka 35 akifanya shughuli za uhifadhi katika hifadhi ya Serengeti. 

Mradi wa mbwa mwitu Serengeti unaendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, TANAPA na Chuo Kikuu cha Glasgow.

1 comment:

Anonymous said...

Mimi si mtaalam lakini moja ya sababu kubwa mbwa mwitu kuhama au kukimbia makazi yao ni mwanadamu. Katika uchunguzi uliofanywa nchini India ambao wanambwa mwitu vile vile imegundulika wakaazi wanaoishi karibu na maakazi yanayowahifadhi mbwa mwitu wanatabia ya kufuatilia nyendo za mbwa mwitu katika mawindo yao ili kuwatimua baada ya kwisha kuua myama kwa ajili ya chakula chao na mwanadamu kujichukulia huo mzoga kirahisi baada ya kazi kubwa iliokwisha kufanywa na mbwa mwitu kutokana na tabia hiyo mbuvu ya
mwanadamu ndipo mbwa mwitu wanapoamua kuyakimbia makazi yao hasa kutokana na kushinda na njaa kwa muda mrefu baada ya binaadamu Kuwanyang'anya msosi wao. Na ushahidi yakuwa inawezekana ikawa ndio sababu iliyowakimbiza hao mbwa mwitu katika hifadhi ya taifa ni pale tunapoona kwenye YouTube wananchi wa jamii ya kimasai wanapokwenda kupambana na simba ili awaachie mnyama alieua simba kwa ajili ya chakula chake.sasa kama mwanadamu anadiriki kwenda kumnyanganya simba msosi wake vipi mbwa mwitu? Inasemekana kitendo cha mbwa mwitu kunyanganywa mnyama waliokwisha kumuua kinawaudhi sana na kuwakatisha tamaa pengine hii sio sababu kubwa iliowafanya hao mbwa mwitu kukimbia katika hiyo hifadhi isipokuwa wahusika wanatakiwa kutafuta sababu la sivyo hao mbwa watatoweka tena katika hayo maeneo.