Wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) wakila kiapo cha Uadilifu kabla ya kujaza fomu za ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa Umma.
Afisa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Umma ndugu Hendry Sawe akitoa mada juu ya Maadili kwa Viongozi wa Umma na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa Umma muda mfupi kabla ya wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kujaza fomu za ahadi ya uadilifu.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), ndugu Elishilia Kaaya akiweka saini fomu za ahadi ya uadilifu za baadhi ya Wafanyakazi wa AICC baada ya wafanyakazi hao kuapa na kuzijaza.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC),
ndugu Elishilia Kaaya akiongea na wafanyakazi kabla ya kuapa na kujaza
fomu za ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa Umma. Katikati ni Mkurugenzi
wa Fedha na Utawala wa AICC, ndugu Savo Mungóngó na kulia ni Afisa
Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Umma, ndugu Hendry Sawe.
No comments:
Post a Comment