Advertisements

Sunday, February 14, 2016

Magufuli hatimaye aitaja Zanzibar

Kwa mara ya kwanza, Rais John Magufuli amezungumzia hali ya kiasia visiwani Zanzibar na kuweka bayana kwamba kamwe hataingilia mgogoro huo kwa kuwa Tume ya Uchaguzi ZEC ina uhuru wa kujiamulia mambo yake kama ambavyo inaona inafaa.

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambao waliomba kuzungumza naye kuhusu mambo mbalimbali aliyoyafanya kwa siku 100 alizokaa Ikulu.

Ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuzungumzia mkwamo wa kisiasa wa Zanzibar licha ya kukutana na viongozi watatu wa juu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) mapema mwaka huu.

Mkwamo huo unatokana na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wawakilishi wa Oktoba 25, mwaka jana akitaja sababu tisa zilizoufanya usiwe haki na huru.

Tangu hapo, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Shariff Hamad na Makamu wa Pili, Balozi Seif Ali Iddi wamefika Ikulu kumueleza maendeleo ya mkwamo huo na kisha kuzungumza wao na waandishi wa habari badala ya Rais Magufuli.

Rais Magufuli ambaye kwenye mkutano wa jana aliambatana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar Ibara ya 115 au 112, ZEC ina uhuru wa kuendesha mambo yake bila kuingiliwa ingiliwa hivyo haoni sababu ya kuingilia suala hilo.

“Tume zote za uchaguzi duniani ziko huru kufanya mambo yake, kama ilivyo huru NEC ya Tanzania bara, ZEC nayo iko huru pia," alisema Rais Magufuli nak kueleza zaidi:

"Kama ni uhuru basi tume zote ziko huru. Haiwezekani tume moja ikawa huru na nyingine ikakosa uhuru wa kufanya mambo yake.”

Aidha, Magufuli alisema yeye anazifahamu na anaziheshimu sheria za nchi hivyo aliwataka viongozi ambao wanaona tafsiri hiyo ya kuipa uhuru ZEC ni mbaya, basi wakatafute tafsiri mahakamani na si kumshinikiza yeye kuingilia masuala ya Zanzibar.

Pamekuwa na shinikizo kutoka vyama vya upinzani, wahisani wa nje na wanaharakati wakimtaka Rais Magufuli aingilie kati mzozo huo wa uchaguzi wa Zanzibar.

Zec imeamuru kuwapo kwa marudio ya Uchaguzi Mkuu Machi 20, mwaka huu.

“Mahakama zipo lakini hamuendi mahakamani na badala yake mnanishikiza mimi niingilie," alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa na wazee waliokuwa wakimsikiliza.

"Nawahakikishia kuwa sitaingilia na nitaendelea kukaa kimya maana jukumu langu kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ni kuhakikisha Unguja na Pemba zinakuwa salama.

“Mtu yeyote ambaye atathubutu kuleta chokochoko iwe Pemba, Unguja, Ukerewe na popote pale basi watajua kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo na vitawashughulikia kikamilifu.”

ZEC ilifuta matokeo ya Uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana ikisema kuwa haukuwa huru na haki kwani baadhi ya taratibu zilikukwa na kwenye baadhi ya vituo vya kupigia kura idadi ya wapiga kura ilizidi idadi ya watu waliojiandikisha.

Uchaguzi huo Machi 20 umesusiwa na chama kikubwa cha upinzani cha CUF na vyama vingine vidogo vidogo.

Mgogoro wa kufutwa kwa matokeo hayo kulisababisha mikutano ya hapa na pale kwa viongozi wa juu wa kitaifa kujaribu kutafuta mwafaka lakini mazungumzo hayo hayakuzaa matunda baada ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CUF, maalim Seif kujitoa mwezi iliopita.

Maalim Seif alijitoa kwenye mazungumzo hayo akisema kuwa ni sawa na kiini macho kwani ZEC tayari ilikuwa na msimamo wake wa kurudiwa kwa uchaguzi huo na CCM ilikuwa ikiwahamasisha wanachama wake kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio wakati mazungumzo yakiendelea.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

5 comments:

Anonymous said...

hawa wazee waliomtakamagufuli waongee nae...... nini walichongea nae mbona hatujakisikia, au ni mgufulia amewataka wazee aelezee alichokuwa nacho.
katika bunge aliahidi suala la zanzibar atalishughulikia, alipokutana na wazee suala la zanzibar hawezi kuliingilia. so how ???????????

Anonymous said...

jamaa tumeanza kumuona mapema kuwa ni msanii, anakuwa na ahadi ambazo hawezi kuzitimiza, alijigamba atashiriki mdahalo, akaingia mitini, ameahidi kuwatumikia watanzania wote na kuwatendea haki, kinachoendelea zanzibar tunajionea wenyewe hata ulimwengu unashuhudia. tutaendelea kuona usanii wak

Anonymous said...

Mdau, hebu funguka.Unataka JPM aingilie swala la Zanzibar kwa namna gani?

Anonymous said...

Wapemba bhana,
Kwakua JPM hakuongea in favor of CUF basi hakuna alichoongea !
Option iliopo sasa hivi ni uchaguzi, nafasi ya mazungumzo ilikuwepo na muda wake ulikwisha.Hatuwezi kuwa na mazungumzo yasiyokwisha.

Anonymous said...

Magufuli ni msanii. Mtamkumbuka JK. Jamaa hana sera zaidi ya kusimamisha watu kazi.