Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majliwa Majaliwa (kulia) akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa Habari kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna.
(Picha zote na Benedict Liwenga)
Na. Immaculate Makilika.
Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri wasiorudisha fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni na fomu ya Ahadi ya Uadilifu wamesisitizwa kurudisha fomu hizo leo kabla ya saa 12 jioni katika ya Ofisi ya Tume ya Maadili iliyopo jijini Dar es salaam na watakaoshindwa kufanya hivyo watakua wamejitoa wenyewe kwenye nafasi zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majliwa ofisini kwake alipokutana na Waandishi wa Habari akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki, ambapo ameeleza kuwa, kufuatia Semina iliyofanyika Februari 25 mwaka huu kati yake na Mawaziri kuhusu Mwongozo wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu, ambapo Kamishna Mkuu, Mhe. Jaji Mstaafu Salome Kaganda alitoa maelezo kwamba kuna baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao hawajarudisha fomu hizo hadi kufikia jana.
Akiwataja Viongzoi hao, Mhe. Majaliwa alisema kuwa, Mawaziri ambao hawajarudisha fomu hizo ni akiwemo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Mhe. January Makamba, ambao wote hawajarudisha fomu za Rasilimali na Madeni na fomu za Ahadi ya Uadilifu, vilevile Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga ambaye hajarudisha fomu ya Ahadi ya Uadilifu, na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, ambaye hajarudisha fomu ya Tamko la Rasilimali na Madeni, pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano, Mhe. Luhaga Mpina ambaye hajarudisha fomu zote mbili.
Mhe. Majaliwa, amewasisitiza Mawaziri hao kujaza fomu hizo kwa kua ni agizo la Mheshimwa Rais kujaza fomu hizo leo kabla ya saa 12 jioni, “viongozi watakaoshindwa kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni na fomu ya Ahadi ya Uadilifu wanatakiwa kujieleza kwa kutoa sababu za kushindwa kufanya hivyo na watachukuliwa hatua” alisema Waziri Mkuu.
Kwa mujibu wa kifungu cha 9 Sheria ya Maadili ya Uongozi wa Umma ya mwaka 1995 sura ya 8 inawataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma (Tamko la Raslimali na Madeni) na fomu ya Ahadi ya Uadilifu mara wanapoteuliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi. Lengo la kujaza fomu hizo ni kuwa na uwajibikaji kwa kiongozi juu ya uadilifu wake wakati wote anapokua mtumishi wa Umma.

3 comments:
Hapa sikubaliani na Magufuli. Kuna issue zingine zinaweza kufanyika kwa ndani bila waandishi wa habari. Kudhalilisha watu kila siku kwenye vyombo vya habari sio utu sio ubinadamu and its not professional. Hawa ni mawaziri kawachagua mwenyewe. This could have been handled internally. There has to be a trust factor and respect btn the president and people he appointed to work for him otherwise he will find himself alone.
Kila anayependekezwa kuchukua nafasi ya uongozi anaelewa kuwa anatakiwa kujaza fomu ya maadili ya utumishi wa umma na kuirudisha kwa wakati mwafaka kwa chombo kinachohusika. Kusudio la fomu hii ni kumthibitisha kuwa kiongozi huyo anafaa kutwaa wadhifa huo alioteuliwa. Kuepukana na shari viongozi wanaopewa nyadhifa zinazoambatana na ujazaji wa fomu ya maadili wanatakiwa wajaze fomu hizo na kuzirudisha kwa wakati unaokubalika na kama kuna yeyote mwenye tatizo au haoni haja ya kuja fomu hizi asikubali uteuzi aliopewa. Hapa ni kazi tu na wakati wakuoneana haya umeisha.
Mdau wa hapo juu hujui unachokiongea Magufuli kabla ya hata hajawa raisi na ningekuomba urudi nyuma kabisa kwenye Campaign zake za uchaguzi nini muheshimiwa Maghufuli aliwahidi watanzania. Moja ya mambo aliokuwa anasisitza ni uadilifu katika baraza lake la mawaziri na serikali yake. Na aliahidi yeye mwenyewe pamoja na mawaziri wake lazima waainishe mali wanazomiliki na utajiri wao kabla ya kuanza kazi ya kuwatumikia watanzania. Hata hao mawaziri walipokubali wito wa Magufuli wa kufanya nae kazi walishajua hilo la kutangaza mali zao linakuja tena hadharani. Tena kudhalishwa na unprofessional gani unakozungumzia kama si wewe mwenyewe binafsi kutofahamu unachokizungumza. In open Governance the way mr Magufuli is running his government there's no such thing called handling of internal affairs secretly. He promised the people that he will let them know each and every step their government is taking in almost every day life. He promised the people he will order his ministers and other deputies to declare their properties openly and this is what exactly doing right now and i myself as Tanzanian i can't thank him much except im proud of him every minute for the the heck of the job is going right in Tanzania.
Post a Comment