ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 21, 2016

MBUNGE ALLAN KIULA WA IRAMBA MASHARIKI AAGIZA VIONGOZI WALIOUZA CHAKULA CHA MSAADAA WAKAMATWE

 Mmoj ya wananchi waliohudhuria kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki kumsikiliza alipokuwa akizungumzia masuala ya maendeleo ya jimbo hilo.
 Wananchi waliohudhuria kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki kumsikiliza alipokuwa akizungumzia masuala ya maendeleo ya jimbo hilo.
 Wananchi waliohudhuria kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki kumsikiliza alipokuwa akizungumzia masuala ya maendeleo ya jimbo hilo.
 Mbunge wa jimbo la Iramba mashariki(CCM)Bwana Allani Kiula (aliyeshika karatasi) akitoa maagizo ya kukamatwa kwa viongozi waliouza chakula cha msaada katika Kijiji cha Nkungi,tarafa ya Nduguti,wilayani Mkalama.


SERIKALI wilayani Mkalama,Mkoani Singida imemuagiza afisa mtendaji wa Kata ya Ilunda,tarafa ya Nduguti kuwasaka na kuwakamata mara moja viongozi wa Vijiji na Vitongoji wanaotuhumiwa kuuza chakula kilichotolewa msaada na serikali kwa watu wanaokabiliwa na tatizo la njaa kwa bei ya shilingi 2,000/= badala ya shilingi 1,000/= kwa kilo 20. 
 Agizo hilo limetolewa na Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki,Allani Kiula kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nkungi, kufuatia malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wananchi kwamba licha ya chakula hicho kutakiwa kuuzwa kwa bei ya shilingi 50 kwa kilo lakini wamekuwa wakiuziwa kwa bei ya shilingi 2,000/=. 
 Kwa mujibu wa mbunge huyo kutokana na chakula hiho kuuzwa kwa bei ya juu kuliko walivyotegemea,idadi kubwa ya wananchi hao wamekuwa wakipata taabu ya kukinunua,jambo ambalo limewaumiza kwa sasa kutokana na kutokuwa na fedha katika kipindi hiki kigumu wanachokabiliana na tatizo hilo la njaa. 
 Kwa upande wake mmoja wa watu wenye ulemavu wa viungo,Eliasi Manya akitoa malalamiko hayo kwa Mbunge huyo alisema kwamba kutokana na kukosa chakula hicho cha msaada huku wao wakiwa hawana uwezo,kumechangia wao kuishi maisha ya kuombaomba huku wakiwa hawana uhakika wa hata mlo mmoja wa chakula.
“Juzi tumepewa posho hapa tuliambiwa posho hii inauzwa kwa kilo shilingi hamsini,ajabu nilipewa debe moja nikawa nimelipa shilingi elfu mbili sijui ndiyo nimenunua hela ngapi kwa kilo moja sijaelewa”alifafanua mzee huyo. 
 Hata hivyo Manya hakuishia kulalamikia suala la chakula cha msaada peke yake bali alizungumzia pia kitengo cha kunusuru kaya maskini kwamba baada ya kupokea fedha zinazotolewa na mfuko huo walitakiwa kukatwa shilingi 10,000/- kila mmoja kwa ajili ya kujiunga na Mfuko wa afya ya jamii (CHF ). 
 Alifafanua zaidi mwananchi huyo alibainisha kwamba licha ya kukatwa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kunufaika na huduma za matibabu,lakini mpaka sasa wanapokwenda hospitalini watakiwa kulipa shilingi 30,000/=,jambo ambalo alishindwa kufahamu zile alizokatwa zimeingia katika mfuko gani. 
 Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kiduguwi, Christopher Gyunda anayetuhumiwa kuuza chakula hicho cha msaada kwa bei kubwa,licha ya kukiri kuuza chakula hicho kwa bei ya shilingi 800 badala ya shilingi 50 kwa kilo,lakini alikanausha kuhusika na tuhuma zilizoelekezwa kwake kwamba ameuza chakula hicho kwa bei ya shilingi 2,000/=

No comments: