ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 25, 2016

MWANAMUZIKI MKONGWE KASSIM MAPILI AFARIKI DUNIA LEO

 Mzee wetu Mzee Mapili (Pichani) amekutwa amefariki nyumbani kwake baada ya kutoonekana hajatoka Chumbani kwake kwa Muda Mrefu. Baada ya kuona kimya kimekuwa kingi ndipo majirani hao waliamua kuvunja mlango wa nyumbani kwake eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es salaam na kukuta Mzee wetu akiwa ameishafariki.
Mzee atakumbukwa kwa Kibao cha "Napenda Nipate Lau Nafasi" na "Rangi Ya Chungwa" na vingine nyingi. Pia alikuwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania Dance Music Association ama Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA). 
Mara ya mwisho hadharani Marehemu Mzee Kassim Mapili alionekana akiongoza wanamuziki katika mazishi ya mwanahabari nguli wa burudani Marehemu Fred Mosha katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam, ambako pamoja na kushirki mazishi aliimba kwa hisia beti kadhaa za kumuenzi marehemu Fred.
Taarifa zaidi za msiba huu mzito  zitawajia kadri zitavyopatikana.
Kwa mawasiliano zaidi kwa wasanii wa Tanzania piga namba 0744150000 
 Nawaomba wanamuziki wote Tujitoe 
kwa wingi kumpa heshima Mzee wetu Kassim Mapili....!! 

Imetolewa na Addo November
 Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania..!!

No comments: