ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 11, 2016

NIWE NA NANI 30


SONGAA..nilipo waona tu wote wakaachiana kama vile wamenasuliwa kwenye shoti ya umeme alafu wakainamisha vichwa kama kondoo..Baada ya fumanizi zito lile ambalo kama ingekuwa ni mke wa mtu basi wangeenda kutoa maiti kama mnavyojua mke anavyoumaa... Nilipita na mia kama sio mimi niliye shuhudia tukio lile nikaenda hadi kwenye meza ya chakula kufika hakuna chakula chochote nilikasirika sana kutokukuta chakula na hata dalili ya kupikwa hakuna inaonesha hata jiko limenuna huko.. "ina maanaa ester hajapika na anafanya uchafu wake na baba pale"nikajisemea kwa jaziba ila sikutaka makuu nililiendea friji lililokuwa pale kwenye kile chumba cha kulia nikatoa mkate na juice kisha nikanywa nilipo maliza nikatoka na kupita pale sebleni tena sijawakuta nikaelekea chumbani kwangu moja kwa moja nikajilaza nikiwa na mawazo lukuki bado tendo nililofanya na jenifer lilikuwa limechukua nafasi katika ubongo wangu ila nikalala tu ..

Nakuja kustushwa na sauti ya mama iliyokuwa ikiniita mlangoni..
"kendrick mwanangu kedrick amka nimerudi"nisauti ya mama iliyopenya hasa kwenye tundu za masikio yangu hapo nikaamka nikiwa mwenye furaha mana nimechukuliwa kama mtoto wa nyumba hiyo japo napewa mshahara lakini jinsi mama anavyonijali kama mwanae wa kumzaa kabisa niliamka nikiwa mchangamfu hadi kufika mlangoni kwangu na kufinya kitasa kikafunguka lakini kutoka mama hayupo kashaenda kukaa kwenye masofa na mimi nikaenda hadi pale alipokaa ambako kuna mizigo alafu na mfuko ile ya supermarket...
"shikamoo mama"
"marahaba mwanangu"
"za huko ulipotoka mama"
"salama sana kazi zinaenda mwanangu"
"sawa mama karibu nyumbani sisi tupo muda wote"
"sawa mwanangu embu beba hii mizigo peleka store alafu urudi hapa umesikia mwanangu"nilimwitika huku nashauku ya kujua anachoniitia nikaanza kubeba ile mizigo ambayo ulikuwa ni mkungu wa ndizi pamoja na kiroba ambacho nikagundua ni cha mchele.. Nilibeba kimoja moja pale hadi kuingiza vyote store kisha nikarudi na kukaa pale kochini aliponiita mama nikikaa mkao wa kula ili kujua alichoniitiaa...
"mwanangu si unakumbuka wakati naondoka nilikwambia nini"
"ulisema sijui utaniletea nini dah nimesahau mambo mengi mama"nikajifanya nimesahau
"ahaa sawa mwanangu nilikwambia nitakuletea zawadi si ndio umekumbuka eeh"
"ndio mama nimekumbuka kabsa "nikajifanya ndio nimekumbuka..
"zawadi yako hii hapa "alinipa mfuko mama huku akiniambia niangalie na mimi nikaangalia nikakuta boksi lenye picha ya simu aina ya samsung galaxy nilishangaa sana nikalitoa upesi upesi na kufungua ile kufungua sikuamini macho yangu kuikuta simu ambayo ilikuwa juu ya boksi nilifurah kimoyo moyo...
"asante sana mama nashukuru sana kwa zawadi yako nimeipenda mungu akubaliki mama"nikajikuta maneno yanitoka mfurulizo..
"sawa mwanangu asante na wewe kwa ufanyaji kazi wako nashukuru mungu kupata kijana kama wéwe mwenye msimamo na kazi zako"
"sawa mama nashukuru"nilimwambia mama wakati huo kiza ndio kinamea hata chakula hajijapikwa bado ila ester yupo jikoni anapika... Mama aliniaga na kwenda chumbani kwake.... nilianza kuikagua siku kwa kuiangalia kama mtu nisie amini kumiliki simu ambayo sijawah kuwaza kuwa nayo niliishia kuwaona nazo watajiri tu au watu wenye pesa zao baada ya kuikagua nikaelekea chumbani kwangu mana nilikumbuka mama kaniambia nichaji kabla ya kutumia nikaweka chaji huku ikiendelea kuingza chaji nikatoka nje pale sebleni kuangalia tv nikiwa nimekaa naangalia tv akaingia jenifer...
"hi my kendrick"ni sauti ya jenifer nikamwangalia na kutabasamu kisha nikaitikia salamu ya kimombo.
"nimekumis kweli yani we acha tu yani nipo njiani lakini mawazo yote kwako"alisema jen bila woga japo alikuwa na taarifa ya ujio wa mama yake
"mimi pia jen nimekumis kwel "mazungumzo yaliendelea huku tukicheka na kupiga story kisha akaniaga na kuingia chumbani kwake wakati huo ester kaivisha tukaitwa wote hadi meza ya chakula kisha kila mtu akajiwekea kama kawaida ya siku zote na kuanza kula huku stori zikiendelea jambo lililo ni shangaza kweli watu wengine hawana haya yani baba alikuwa akiuonesha upendo bandia kwa mama eti anamlisha anajifanya anampenda kumbe anatoka na ester kila wakati baba ananiangalia kwa macho ya kutisha ila napotezea tu sikumjali tulikula hadi wote tulipo maliza kila mtu akanawa tukala matunda alafu wote tukaingia vyumbani kwetu mimi nilipoingia sehemu ya kwanza kuangalia ni kwenye simu nilifika hadi ilipo nikaiwasha bahati nzuri ishawekwa line yenye uwezo 4G hakuna majina ya simu alafu zikaingia msg za tigo zenye ofa nilifurah na kuanza kuichezea kisha nikalala..
Hadi kulipokucha nikatoka nje na kwenda kwenye kazi nikiwa naendelea pale jen akatokea na kuniambia nikavae twende dukaniakafu tupitie beach nikaenda ndani haraka kuvaa ila simu nikasahau kisha nikatoka na kumfata jen tukaingia ndani ya gari likatoka tulifka hadi shooping na kutoka kwenye gari jen akawah kutoka.. Sasa ile nataka kutoka mimi kabla sijafika alipo jen ikaja teksi ikasimama na kuniteka wakaniingza ndani..
ITAENDELEA

No comments: