Advertisements

Saturday, February 6, 2016

POLISI INDIA YASIMAMISHA KAZI POLISI WAWILI WALIOKUA KWENYE TUKIO WAKATI MWANAFUNZI MTANZANIA AKIDHALILISHWA

Photo published for India mob beats, partly strips Tanzanian student - Capital News
Na Mwandishi wetu Vijimambo Blog.

Mamlaka ya Polisi mji wa Bangalore nchini India imewasimamisha kazi Polisi wawili kutokana na tukio la kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa miaka 21 Mtanzania aliyedhalilishwa kwa kuvuliwa nguo kitendo kilichofanywa na kundi la wananchi wenye hasira baada ya kutokea kwa ajali ya mwananchi mwingine rsis wa Sudan kumgonda mwanamke mwenyeji wa eneo hilo na kusababisha kifo chake na yeye kusalimisha maisha yake kwa kutokomea kusikojulikana.

Kitendo cha kumvua nguo msichana mwanafunzi wa Kitanzania na kisha kumpiga, Serikali ya India inakichukulia kama ni cha kuitia aibu nchi hiyo.

Kundi la watu lilimshambulia msichana huyo aliyekua akiendesha gari eneo hilo la kusini mwa jimbo la Kamataka siku ya Jumapili Januari 31, 2016 akiwa na wenzake kwa kumpiga na kumchania blauzi yake huku wakichoma moto gari waliyokua wakiendesha.


Polisi wa Bangalore imesema jana Ijumaa Februari 5, 2026 imewakamata watu wengine 4 usiku wa alhamisi na kufanya idadi ya watu wanaoshikiliwa na Polisi kutokana na tukio hilo la udhalilishaji la mwanafunzi Mtanzania kufikia 9.

Polisi wawili waliosimamishwa kazi ni wale waliokua kwenye eneo la tukio na kushindwa kuzuia kundi lililokua likifanya unyanyasaji wa mwanafunzi Mtanzania aliyekua akiendesha gari lake akiwa na wenzake karibu na eneo hilo.

Mwanafuzi wa Kitanzania aliyepigwa na kudhalilishwa na kundi hilo akifanya mahojiano na luninga ya The Tmes ya India alisema Gari lao lilichomwa moto na wao kupigwa akiwemo yeye kuchaniwa baluzi yake japo walijaribu kukimbia kusalimisha maisha yao kwa kujaribu kupanda basi lakini cha kushangaza Dereva wa basi hilo alilisimamisha na wao kushushwa kwenye basi huku wakiendelea kupigwa na kundi hilo.

Mwananfunzi huyo alizidi kuiambia The Times ya India kwamba yeye alikua hafahamu lolote kuhusiana na ajali hiyo ya Msudani kwamba yeye na wenzake walikua wakipita njia kwenye eneo hilo na kukutana na yaliyowakuta.

Balozi wa Tanzania nchini India Mhe.John Kijazi kwenye mahojiano yake na gazeti la Express la nchi hiyo amesema shambulio la mwanafunzi huyo limetokana na yeye kuwa mwafilika kwani wakati ajali inatokea mwanafunzi huyo wa Tanzania hakuwepo eneo hilo na wala hakujua chochote kuhusiana na ajali hiyo ya Msudan, kushambuliwa kwao imetokana na rangi yao ya Uafrika.

Wanafunzi wa Kiafrika walikua wakitumiwa ujumbe wa kibaguzi siku mbili mfululizo tangia siku ilipotokea tukio hilo na kusababisha wanafunzi kujifungia ndani kwa kuhofia usalama wao. 

1 comment:

Anonymous said...

Kwani wahidi wanataka tuwafukuze Tanzania?!!! Sheria kali zichukuliwe dhidi ya waarifu hawa. Na Hisitokee tena uwe mwisho. Maana tutawachana chana wahindi wote Tanzania wasituchezee kabisa. Sisi sio wajinga.