Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi
watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa.
Rais Magufuli pia
amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.
Vituo vya
uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia
kukamilika.
Kwa upande wa
Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
1.
Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa
cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum
ya Dar es salaam. Kamishna Sirro
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
2.
Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa
cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na
Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve
aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
3.
Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye
amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya
Intelijensia. Kamishna Mikomangwa
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
4.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi Nsato Marijani Mssanzya
ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara
ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna
Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses
Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Aidha, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya
Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika
Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba
anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Teuzi zote
zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
15
Februari, 2016
6 comments:
Dr Migiro, from UN to Ambassador, hapo iko kazi
But hawa tuliwatosa kwenye uchaguzi? Very interesting.
KUMBE USIPOKUWA DOCTOR AU PROFESSOR KATIKA NCHI HII UNAITWA MHESHIMIWA? SASA HUYO CHIKAWE HANA UWAZIRI WALA UBUNGE BADO ANAITWA MHESHIMIWA KAMA VILE NI CHEO.....KUMBE NDIYO MAANA KIKWETE ALIKOMALIA APATE UDAKTARI MWINGI WA FALSAFA WA KUPEWA ILI AITWE MHESHIMIWA HATA ANAPOMALIZA MUDA WAKE. HAO WOTE WALIKATALIWA NA WAPIGA KURA WAO, WENGINE WALIFANYA VIBAYA KATIKA VYEO WALIVYOPEWA WAKAACHWA LAKINI LEO WANAPEWA VYEO VIKUBWA TENA. KWELI HII NI TANZANIA.
Migiro aliyekuwa bubu UN hakuna asiyemjuwa
Leo balozi CCM Kweli uozo
Magufuli jitumbue majipu mwenyewe
Hakuitangaza Tanzania akiwa UN leo ataweza
Fyuuuuuuuu
Kubebana huku
Rais JPM kama ni kuteua mabalozi basi hapomkwa Dr. Asha Rose ndio umechemka. Kwa sisi tuliokaaa naye tunamjua. Na aliondoka kwa aina fulani ya kutowajibika na kuja kupewa nafasi kwenye bunge la katiba! Kama zawadi toka kwa Kikwete na leo tena Balozi. Hahh tusubirie hiyo posti lakini mtakaopewa mjue kazi iko!! ()..
Post a Comment