ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 15, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ATEUA MABALOZI WATATU NA MAKAMISHNA WANNE WA JESHI LA POLISI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya  Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau. 
 Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.
Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
1.      Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
2.      Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
3.      Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Intelijensia. Kamishna Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
4.      Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato Marijani Mssanzya ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

15 Februari, 2016 

6 comments:

Anonymous said...

Dr Migiro, from UN to Ambassador, hapo iko kazi

Anonymous said...

But hawa tuliwatosa kwenye uchaguzi? Very interesting.

Anonymous said...

KUMBE USIPOKUWA DOCTOR AU PROFESSOR KATIKA NCHI HII UNAITWA MHESHIMIWA? SASA HUYO CHIKAWE HANA UWAZIRI WALA UBUNGE BADO ANAITWA MHESHIMIWA KAMA VILE NI CHEO.....KUMBE NDIYO MAANA KIKWETE ALIKOMALIA APATE UDAKTARI MWINGI WA FALSAFA WA KUPEWA ILI AITWE MHESHIMIWA HATA ANAPOMALIZA MUDA WAKE. HAO WOTE WALIKATALIWA NA WAPIGA KURA WAO, WENGINE WALIFANYA VIBAYA KATIKA VYEO WALIVYOPEWA WAKAACHWA LAKINI LEO WANAPEWA VYEO VIKUBWA TENA. KWELI HII NI TANZANIA.

Anonymous said...

Migiro aliyekuwa bubu UN hakuna asiyemjuwa
Leo balozi CCM Kweli uozo
Magufuli jitumbue majipu mwenyewe

Anonymous said...

Hakuitangaza Tanzania akiwa UN leo ataweza
Fyuuuuuuuu
Kubebana huku

Anonymous said...

Rais JPM kama ni kuteua mabalozi basi hapomkwa Dr. Asha Rose ndio umechemka. Kwa sisi tuliokaaa naye tunamjua. Na aliondoka kwa aina fulani ya kutowajibika na kuja kupewa nafasi kwenye bunge la katiba! Kama zawadi toka kwa Kikwete na leo tena Balozi. Hahh tusubirie hiyo posti lakini mtakaopewa mjue kazi iko!! ()..