Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za pole Mke wa
Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na ajali ya gari, iliyotokea jana
tarehe 08 Februai, 2016 akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.
Ajali hiyo
imetokea katika eneo la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari
aliyokuwa akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha
pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.
Katika salamu hizo
alizozituma kupitia kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter
Pinda, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali
hiyo na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.
"Kupitia
kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo
Mama Pinda kwa kuumia katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye
majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku"
alisema Rais Magufuli.
Mama Tunu Pinda anaendelea
kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
09
Februari, 2016
No comments:
Post a Comment