ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 24, 2016

SERIKALI NA AKDN WAJADILIANA KUBORESHA MKATABA WA USHIRIKIANO

Maafisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika kikao cha pamoja na Taasisi ya Maendeleo ya Aga Khan (The Aga Khan Development Network- AKDN). Wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine ambaye alifungua rasmi kikao hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz P. Mlima. Kushoto kwa Balozi Sokoine ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka H. Luvanda ambaye aliongoza mazungumzo kwa upande wa Serikali ya Tanzania. Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kilipitia upya Mkataba wa Ushirikiano wa Kimaendeleo kati ya Serikali na AKDN ambao ulisainiwa mwaka 2001. 
Kiongozi wa Ujumbe wa Mtandao wa Maendeleo wa Agakhan Dkt. Shakif Sachedina wa kwanza kushoto ambaye aliongoza mazungumzo kwa upande wa AKDN akiwa na baadhi ya wajumbe wakifuatilia mazungumzo ya kikao. 
Sehemu nyingine ya wajumbe wa AKDN wakifuatilia kikao. 
Wajumbe wa Serikali ya Tanzania walioshiriki kikao hicho ambapo Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa ilikuwa mwenyeji. Ujumbe wa Serikali ulihusisha Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU); Mamlaka ya Mapato Tanzania; Ofisi ya Rais Ikulu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Wizara ya Sera na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Balozi Joseph Sokoine akiagana na wajumbe wa AKDN baada ya kukamilisha zoezi la ufunguzi wa kikao hicho. 

No comments: