
Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige
Serikali ya Tanzania imesema kuwa inaendelea kufatilia ili kuchukua hatua zaidi juu ya matukio yalitokea nchini India katika chuo cha Acharya Bangalore, ikiwemo la mwanafunzi wa Kike kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo.
Akitoa tamko la Serikali leo Bunge Mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige amesema tayari serikali imeshapeleka dokezi la kidiplomasia kwa serikali ya india ili kuonyesha kukasirishwa na kitendo hicho.
Balozi Maige ameongeza kuwa tayari wameitaka serikali ya India kuchukua hatua za kipolisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kupeleka ulinzi wa kutosha katika maeneo wanaoishi wanafunzi hususani wa kitanzania ambapo leo kumeri kwa mtu anaesadikiwa kuwa mtanzania kufariki katika mazingira ya kutatanisha.
Kwa upande wa baadhi ya wabunge wameiomba serikali kuwa na tamko rasmi la kuonyesha kuchukizwa na ubaguzi kwa watanzania pindi waendapo kuishi nje ya Tanzania.
Tukio hilo limekuja baada ya Gazeti la Deccan Chronical la Bangalore kuripoti kuwa tukio hilo limetokea baada ya mwanafunzi raia wa Sudan, Ismail Mohammed kugonga gari la raia mmoja wa india mkazi wa Hessaraghata aliekuwa na Mkewe na kusababisha kifo cha mama huyo.
Wakati huo huo Wanaume wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika kumshambulia na kumvua nguo mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania wamekamatwa, shirika la habari la AP limeripoti.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj, aliandika kwenye Twitter kwamba amesikitishwa sana na “kisa hicho cha aibu” kilichotokea Jumapili eneo la Bangalore.
Source:EATV
4 comments:
HIYO KULAANI TU HAITOSHI, WAZIRI MKUU WA JIMBO LA KARNATEKA HUKO INDIA ALISEMA KUWA HUYO "MSICHANA MTANZANIA ASINGEDHALILISHWA KAMA HUYO MWAFRIKA MSUDANI ASINGEMGONGA NA KUMUUA MUHINDI HUYO" HAYO NI MANENO YA KIBAGUZI NA YASIYO NA HEKIMA HATA KIDOGO!! JE MTU MWINGINE AKIFANYA KOSA MWINGINE WA RANGI INAYOFANANA ATAKUWA NA KOSA? KWA NINI WATU NA SERIKALI YAKE ITOE "COLLECTIVE PUNISHMENT" KWA HUYO MWANAFUNZI NA WENZAKE WASIYEKUWA NA HATIA?? SERIKALI YETU INAKOSEA SANA....HILO TATIZO LA KUONEWA KWA WATU WA RANGI NYINGINE NA LA RACE (CASTE SYSTEM) NI LA KAWAIDA KWA WAGENI WOTE HALAFU LEO TUNAFIKIRIA KUWASAPOTI INDIA ILI IWE MJUMBE WA KUDUMU KWENYE UNITED NATIONS? ANATAKIWA WAZIRI MAHIGA ASIMAME KWENYE PODIUM ATOE MSIMAMO WA TANZANIA NA JINSI AMBAVYO WATANZANIA WAMECHUKIZWA NA LILILOTOKEA NA AELEZE JINSI GANI AMBAVYO RAIA WA INDIA,WAGENI KUTOKA INDIA NA WAHINDI RAIA WANAVYOISHI KWA AMANI KATIKA NCHI YETU WANAVYOISHI KWA AMANI BILA KUBAGULIWA. KUTOA "VERBALE NOTE" PEKEE KWA SERIKALI YA INDIA BADO HAITOSHI NA SIDHANI KAMA HILO NI SULUHISHO KWA SABABU HAYA MATATIZO YANAJIRUDIA RUDIA KILA MARA HUKO INDIA NA MAPOLISI WALIOKUWEPO BADALA YA KUMUOKOA HUYO MSICHANA MTANZANIA WAO WALIKUWA WAANGALIAJI TU KITU AMBACHO KINAONYESHA WALIKUWA WAKIPENDEZWA NA KILICHOKUWA KIKITOKEA.
watoto wenu wakibaguliwa katika nchi za watu inakuwa isue, watanzania wenzenu muna wanyanyasa na kuwatesa ndani ya nchi yao kama hawana haki ya nchi yao, hii ndio dhambi ilioelezwa na mwalimu nyerere, ukimbagua mtu na wewe utabagukiwa
Anony, wa 6:18 PM, nakuuliza kama wewe ni mwarabu au mhindi? Unaweza kurudi India au Uarabuni ulikotoka au Vizazi vyako vilitoka, hulazimishwi kuishi Tanzania. Sisi hatuna ubaguzi, sielewi hilo usemalo kama linalo ushahidi. Kama unao ushahidi, basi peleka suala lako Wizara ya Sheria, watakusaidia. Usichanganye hili suala la hao "Indian Thugs" na jingine lolote. Tunao Wahindi wengi nchini, na kama Waafrika tutaanza kuwabagua na kuwadhalilisha, basi kilio kikubwa kitawapata wahindi.
Too sad!
Post a Comment