ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 3, 2016

SIDA WARIDHISHWA NA MIRADI YA REA

2
Mtambuzi wa miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijini, Mhandisi Elneema Mkumbo akitoa maelezo juu ya utekelezaji wa miradi ya REA, kwa Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden( SIDA) Maria Van Berlokom ( aliyeweka mikono kifuania) ambao ni miongoni mwa wafadhili wa miradi hiyo akiwa na ujumbe wake pamoja na wadau wengine wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ujerumani( GIZ) wakati wakikagua utekelezaji wa miradi ya REA katika mikoa ya kanda ya kaskazini.
1
3
4
5

Muonekano wa nyumba zilizounganishwa na huduma ya umeme unaotekelezwa na Wakala wa Nishati vijijini REA katika kijiji cha Kwedizinga mkoani Tanga. 



Na Mwandishi Wetu 

Shirika la Kimataifa la maendeleo la Sweden( SIDA), limeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya Umeme inayofahiliwa na Shirika hilo hususan usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini REA kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini( Tanesco), katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la maendeleo la Sweden( SIDA) Maria Van Berlekom amesema hayo mara baada ya kuona maendeleo ya wananchi wa vijijini wakati wa ziara yake ya kutembelea utekelezaji wa miradi hiyo katika mikoa ya kanda ya kaskazini .

3 comments:

Anonymous said...

Sikusudii kuukashifu mradi huu wenye nia njema, lakini naona hii inakaribia kuwa sawa na kuvaa shati lililo chanikachanika na suruali iliyo chanikachanika, kisha unapiga tie na mkandanje!

Kwa nini wasingeanza na mradi wa kuboresha nyumba za wananchi wa vijijini kwanza? Mwananchi, naamini, angefurahi zaidi kuwasha kibatali lakini yumo kwenye nyumba yenye ubora (ya kudumu).

Napita tu!

Anonymous said...

It is even dangerous kuweka umeme hapo!

Anonymous said...

Nakubaliana asilimia 100% na mdau wa 8:59 AM. Hii ni joke kubwa.