Sherehe ya Taleetha Shedrick ya kuhitimu miaka kumi tangu kuzaliwa kwake iliohudhuriwa na ndugu , jamaa na marafiki yafana sana. Sherehe hiyo ilifanyika katika mji wa Laurel, Maryland USA, kwenye hoteli ya Holiday Inn Express & Suites jumamosi ya tarehe 20 mwezi huu wa februari.
pichani Taleetha akiingia ukumbini huku akiwa amesindikizwa na wazazi wake, mama yake mzazi ,Bi Datu na baba yake mzazi, Bwana Shedrick
mama na mwana wakipata Ukodak wa pamoja
Taleetha akipata picha ya pamoja, na binamu zake kutoka London UK waliojumuika pamoja naye kusherekea siku yake ya kuzaliwa.
Taleetha akiimbiwa na watoto wenzake wimbo wa kukata keki na kumtakia maisha marefu yenye afya njema na baraka.
Taleetha akimlisha mama yake, Bi Datu kipande cha keki.
Bibi mzaa baba wa Taleetha akilishwa kipande cha keki na mjukuu wake.
No comments:
Post a Comment