Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Mosses Nnauye akiongea na wanahabari kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya TBC Balozi
Herbart Mrango ambao umefanywa na Rais John Pombe Magufuli,uteuzi huoumeanza
kuanzia tarehe 19/02/2016, kulia ni Mkurugenzi msaidizi Usajili wa magazeti Bw.
Raphael Hokororo
MKUTANO WA MHE. NAPE MOSSES NNAUYE, WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO NA WAANDISHI WA HABARI
TAREHE 20/02/2016
Dondoo za Kuzungumzia;
Napenda kuwafahamisha kuwa kufuatia Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kumaliza Muda wake,
uundwaji wa Bodi Mpya umekamilika. Ni vyema kuwafahamisha kuwa katika utaratibu
wa kisheria wa kuunda Bodi ya TBC mwenye Mamlaka ya kisheria ya Kumteua
Mwenyekiti wa Bodi ni Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.
Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana aliyekuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya TBC iliyomaliza muda wake, Prof. Mwajabu Possi na wajumbe wake wote
kwa kazi waliyoifanya kwa muda wote wa uhai wa bodi hiyo. Ninaamini Bodi Mpya
itaendeleza yale mazuri yote yaliyofanyika na Baodi iliyopita na kubuni mambo
mengine mapya ili kuongeza tija kwa Shirika.
Baada ya kutoa maelezo haya ya awali, sasa nichukue fursa
hii kuwajulisha yafuatayo;
1. Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Mhe. Balozi Herbert E. Mrango (pichani) kuwa
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya TBC. Uteuzi huu unaanza tarehe 19/02/2016 kwa
kipindi cha miaka Mitatu.
Balozi Mrango kielimu ana
shahada ya Uzamili katika uendelezaji wa Mifumo (MSc – Systems Development)
aliyoisomea Chuo Kikuu cha Dublin Nchini Uingereza. Aidha amehitimu Shahada ya
kwanza ya Takwimu za Kiuchumi katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Tanzania.
Balozi Mrango alishashika
nyadhifa mbalimbali, zikiwemo kuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Miundombinu Kuanzia Februari, 2011 hadi
September, 2013.
Nachukua fursa hii
kumpongeza Mhe. Balozi Mrango kwa kuaminiwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huu muhimu. Aidha nimhakikishie Mwenyekiti
huyu Mpya wa TBC kwamba kwa kuwa Shirika la TBC liko chini ya Wizara yangu,
tutampa ushirikiano wa kutosha ili kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika
shirika letu la Utangazaji.
2.
Kwa mujibu wa Sheria iliyounda TBC, baada ya Mhe. Rais kumteua
Mwenyekiti wa Bodi, Waziri mwenye dhamana na shughuli za utangazaji, anateua Wajumbe sita wa Bodi. Katika uteuzi
wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilishatupatia
vigezo vya utaalamu wa wajumbe wakati wa uteuzi.
Hivyo basi, mimi Nape
Moses Nnauye, nikiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, kwa
kuzingatia vigezo vilivyobainishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kwa kufuata
taratibu zingine za kufanya uteuzi, nimewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya
TBC;
(i)
Bw. William Steven Kallaghe; Mtaalamu wa Uchumi.
(M.A – Economics; Head of Public Policy: NBC Bank
Tanzania ).
(ii)
Bw. Mustapha Kambona Ismail; Mtaalamu wa Sheria.
(LLB - UDSM; Associate Director,
Litigation & Investment – Bank of Tanzania; Advocate of the High Court of
Tanzania).
(iii)
Bi. Elimbora Abia Muro; Mtaalamu wa
Uhasibu. (CPA, MBA: Senior Internal Auditor, Tanzania
Investment Centre).
(iv)
Bw. Mick Lutechura Kiliba; Mtaalamu wa Rasilimali
watu. (MBA – Public Service Mgt;
Director of Management: President’s Office – Public Service Management).
(v)
Dkt. Ayub Rioba; Mtaalamu wa Sekta ya Utangazaji
na Utangazaji. (PhD – Mass
Communication; Associate Dean: School of
Journalism, University of Dar Es Salaam) na
6. Bw. Assah
Andrew Mwambene; Mtaalamu wa Sekta ya Habari. ( MSc – Media Research and Analysis; Director of Information: Ministry of Information, Culture, Arts and
Sports).
Uteuzi wa wajumbe hawa ni
kuanzia tarehe 19/02/2016 kwa muda wa miaka mitatu.
3. Nimalizie kwa kuwapongeza tena wote waliopata uteuzi
huu. Tuna matumaini makubwa toka kwao kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa TBC
katika tasnia ya Utangazaji katika ulimwengu wa Teknolojia inayobadilika kwa
kasi kubwa duniani. Ni imani yangu kwamba Bodi hii mpya italeta msukumo mpya
katika utendaji wa Shirika ili hata watumishi wanaofanya kazi katika shirika
hili waendelee kujivunia kuwa ndani ya TBC lakini pia Umma wa Watanzania
wajivunie viwango vya utendaji wa Shirika hili.
No comments:
Post a Comment