ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 22, 2016

TCRA YAIFUNGIA VIDEO MPYA YA WIMBO YA ZIGO REMIX’ YA AY

Ambwene Yessaya ‘AY’ amethibitisha kupokea taarifa ya kufungiwa kwa video ya wimbo ‘ Zigo remix’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz.
Akizungumza na 225 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Jumatatu hii, AY amesema alipokea barua yenye amri hiyo kutoka kwa rafiki yake ambae anafanya kazi katika chombo kimoja cha habari.
“Sijaelewa maadili gani kwa sababu kama maadili niliyokosea mimi ni kushoot kwenye swimming pool, na kama kwenye swimmig pool watu nimevalisha jeans au maturubai hapo nitakuwa nimekosa maadili,” alisema AY.
“Mavazi ya kwenye swimming pool yako kila mahali, hata kwenye taarifa za habari (Michezo) wanaonyesha waogeleaji, kama hiyo pia ni kukiuka maadili ni sawa. Inashangaza mamlaka zetu wanafocus kwenye kufungia nyimbo zetu na kuacha video za nje. Sijawahi sikia muziki wa Kenya, Uganda au Marekani umefungiwa, kama wanaona nyimbo za Nicki Minaj zina maadili halafu Zigo ya AY haina maadili baasi unaacha tu iwe hivyo ,” aliongeza AY.
Pia AY alisema barua hiyo ilitoka kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ikisema kwamba video hiyo inakiuka maadili.
Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi, amethibitisha kuvitumia vituo vya luninga nchini taarifa ya namna ya kupembua kazi za wasanii zisizo na maadili.

2 comments:

Anonymous said...

TCRA ni JIPU, watu wanafanya kazi kama bendera tu. SO SAAAD

Anonymous said...

BWANA MUNGI, HUWEZI UKAMFANYA KILA MTU MTOTO MDOGO. UNAFUNGIA MZIKI KWA SABABU IPI HASA? NAWEZA KUKUBALIANA KUWA MZIKI HUU SIO WA WATOTO KWA HIYO WASIRUHUSIWE, ILA NI WAJIBU WETU KUFIKIRI ZAIDI YA KUFUNGIA TUU. WASOMI MLIOPO TCRA TENGENEZENI MBINU BORA ZA KUCHUJA MIZIKI NA HATA FILAMU, NA SIO KUZUIA WATANZANIA WOOTE WASIPATE BURUDANI KWA KISINGIZIO CHA MAADILI. WASOMI MLIOPO TCRA MUACHE KURAHISISHA MAMBO, KAENI CHINI MMBUNI MBINU MBADALA, TUACHE KURAHSISHA MAAMUZI, BILA KUJALI ATAHRI KWA WASANII. KWA KIFUPI HATA KWENYE NCHI ZILIZOENDELEA KUNA MIZIKI YA KIKUBWA NA YA KITOTO, NA KWA KUTHAMINI UHURU WA WATU WAZIMA KUAMUA, MIZIKI HII HUBEBA TAADHARI, NA KILA MTU ATAANGALIA VIDEO AU KUSIKILIZA MZIKI AKIPIMA YEYE MWENYEWE, SIO LIJIDUBWANA KAMA TCRA LINAJIAMULIA KUFUNGIA MUZIKI WA WATU YAANI HATA WAZEE SISI HATUNA HAKI YA KUSIKILIZA MZIKI HUO? VIPI SANAA NA UBORA WA LUGHA YA PICHA ULIOTUMIKA NAVYO MMEAMUA KUVIUA BILA KUJALI...HUU NI UVIVU WA KUFIKIRI.