ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 16, 2016

UPDATES: PROFESA JOYCE NDALICHAKO AWASIMAMISHWA KAZI MKURUGENZI MKUU BODI YA MIKOPO NA WENGINE WATATU

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amewasitishia mikataba ya kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo (HESLB), George Nyatega na Wakurugenzi wengine watatu kutokana na utendaji mbovu katika kuendesha bodi hiyo.

Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Mikopo ya wanafunzi asimamishwa kazi, wengine ni Mkurugenzi wa Urejeshaji wa Mikopo, Mkurugenzi Upangaji na Utoaji wa Mikopo.

Mkataba wa Mkurugenzi Mtendaji HESLB umesitishwa. Ilikua uishe mwezi August 2016. Mhasibu Mkuu (Bw. Kisare), Mkurugenzi wa Utoaji Mikopo (Bw. Laizer) na Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo (Bw. Chagonja) wamesimamishwa kupisha uchunguzi.

Amewateua wafuatao ku Kaimu nafasi; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mteule ni Bw. Jerry Sabi kutoka Mzumbe University na Kaimu Mhasibu Mkuu mteule ni Bw. Daniel Mafie kutoka NECTA

No comments: