Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki akitangaza kumsimamisha kazi Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Said Nassor pamoja na Kaimu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha, Joseph Mbwilo na Mtendaji wa Chuo cha Tabora Silvanus Ngata wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Chuo
cha Utumishi wa Umma, Said Nassoro (kushoto), akielekea Ofisi kwake, baada
Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki kutangaza
kumsimamisha kazi katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo. (Picha na Loveness Bernard)
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki amemsimamisha kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma Said Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake.
Kairuki ametoa maamuzi hayo leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari katika moja ya kumbi zilizopo katika ofisi za Utumishi wa Umma.
“Namsimamisha Bwana Said Nassoro aliyekuwa mkuu wa chuo hiki kwa kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake na kupelekea suala zima la usimamizi wa shughuli za chuo hususani katika matawi yake mbalimbali yaliyoko mikoani kuathirika,” alisema Mhe. Kairuku.
Kairuki aliongeza kwa kusema kuwa usimamizi wa Bw. Nassoro ambao haukuwa wa ufanisi umetoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhilifu wa mali za Umma ambapo mwaka 2011 na 2013 aliyekuwa mkurugenzi wa chuo upande wa tawi la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi.
Aidha taarifa kutoka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na TAKUKURU zilithibitisha ubadhilifu huo lakini mkuu huyo wa chuo hakuweza kuchukua hatua yoyote badala yake alimuhamisha Bw. Ngata kwenda kwenye tawi la Tabora na kuendelea na wadhifa wake.
Kutokana na ubadhilifu huo imempelekea Kairuki kumsimamisha kazi Bw. Ngata ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora na Bw. Joseph Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za malipo ya ada kiasi cha shilingi bilioni moja ambazo zilikuwa zikilipwa na wanafunzi kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Kairuki ameendelea kueleza kuwa bado wanaendelea kuondoa watumishi wa Umma ambao hawafuati mifumo na miongozo ya Utumishi wa Umma ili kuwabakiza watumishi ambao wanaonyeshe taswira nzuri na kufuata mifumo na miongozo ya Utumishi wa Umma kwa ukamilifu wake.
2 comments:
yani this new gov...kusimamisha kazi na kuwapa deal watu wao is such a indian movie...instead of doing it right they are just media hungry
We mburura wa 5:54pm huoni huyu mkurugenzi ameisananisha hasara nchi ya billioni moja(kama hujui ni million elfu moja)!!! Aliyepewa deal nani hapo. Utawajua mafisadi sasa mnaanza kutoka mapovu. Bado hamjaisoma namba. Hii ni serikali ya wanyonge sisi tunasonga mbele wewe kalagha bhao
Post a Comment