Ben Innes (kulia) akipozi katika picha na mtekaji wa ndege ya Misri, Seif a-Din Mustafa.
-Ni Ben Innes anayeishi Aberdeen
-Picha yake yasambaa kwenye mitandao ya kijamii
-Asema alipiga picha na mtekaji ili auone vizuri mkanda uliodhaniwa kuwa wa mabomu pamoja na kuonyesha tabasamu wakati wa shida
MTU aliyepiga picha na a-Din Mustafa ambaye ni mtekaji wa ndege ya kampuni ya EgyptAir aliyevalia mkanda wa bandia wa mabomu ya kujitoa mhanga amesema kuwa alitaka kuuona vizuri mkanda huo.
Picha hiyo ya Ben Innes, akitabasamu karibu na mtekaji wake katika ndege hiyo ya EgyptAir imesambazwa katika mitandao ya kijamii.
Bwana Innes anayeishi Aberdeen pia aliliambia gazeti la Jumapili la Sun kwamba alitaka kuonyesha tabasamu mbele ya shida.
Alisema kuwa picha hiyo iliyochukuliwa na mfanyakazi mmoja wa ndege hiyo ilikuwa ”selfie bora zaidi”.
Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 55,ikiwemo raia 26 wa kigeni waliotoka Alexandria kueleka Cairo ililazimishwa kutua Cyprus na bwana Seif a-Din Mustafa anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili.
Wengi wa wale waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliwachiliwa huru baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Lanarca lakini mtekaji huyo aliwazuia watu saba kabla ya kisa hicho kukamilika kwa amani.
Polisi nchini Cyprus wanasema Seif a-Din Mustafa – ambaye ana zaidi ya miaka 50 anakabiliwa na mashtaa kadhaa atakapowasili kotini l
BBC
No comments:
Post a Comment