TAARIFA KWA UMMA
UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI YA MCC WA KUSITISHA MAHUSIANO NA TANZANIA YATAWAUMIZA WANANCHI WA VIJIJINI
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeupokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa wa MCC wa kusisitisha mahusiano na Tanzania.
MCC ni Shirika la misaada la Marekani lilianzishwa na Bunge la Nchi hiyo mwaka 2004 kwa lengo la kusaidia miradi ya maendeleo katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa haraka wa uchumi.
Tangu kuanzishwa kwake, shirika hili limesaidia miradi mingi ya maendeleo nchini ikiwemo ujenzi wa barabarani na usambazaji wa umeme vijijini kwa sasa miradi ya aina hiyo inaendelea sehemu mbali mbali hapa nchini na miongoni mwao ni pamoja na mradi wa REA,miradi ya barabara kama ile ya Tnduma Sumbawanga pamoja na Tanga katika barabara ya Horohoro.
Pamoja na vigezo vingine, kigezo mama kwa nchi kufuzu kupata misaada ya MCC ni kwa nchi husika kuzingatia misingi kidemokrasia ikiwemo kufanya uchaguzi ulio huru na haki.
Jana tarehe 28 Machi 2016 Shirika la MCC lilitangaza kusitisha mahusiano na Tanzania kutokana na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM),kubariki kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba 205 na kubariki kurudiwa kwa uchaguzi huo tarehe 20 Machi 2016 katika mazingira ambayo hayakuzingatia misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuvunja matunda ya mwafaka wa kisiasa na kikatiba uliojengwa kwa gharama kubwa visiwani humo.
Chama cha ACT-Wazalendo kinapigania nchi yetu kujitegemea kiuchumi kama msingi wa kujenga utu na uhuru endelevu wa kisiasa na kijamii. Hata hivyo tunatambua kwamba katika kipindi hiki nchi yetu inahitaji mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani, likiwemo shirika la MCC, katika kuendeleza miradi ya maendeleo. Shirika la MCC limekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na kusambaza umeme vijini.
Uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCC utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua na umaskini.
Tunasikitika kwamba ubabe wa Serikali ya CCM na woga wake wa kushindana kidemokrasia umesababisha nchi yetu ikose pesa za MCC ambazo zingesukuma mbele juhudi za kupambana na umaskini.
Tunatoa wito tena kwa Serikali ya chama cha Mapinduzi kuacha ubabe na kufifisha juhudi za miaka ishirini za ujenzi wa demokrasia hapa nchini. Tunatoa wito maalumu kwa wadau wote wa siasa visiwani Zanzibar kurudi mezani na kutatua mgogoro wa kisiasa kwa njia za kistaraabu na katika hali ambayo itarudisha heshima ya nchi yetu katika kukuza demokrasia nchini.
Imetolewa na
Theopister Kumwenda
Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje
29/03/2016
5 comments:
Amka bwana Kumwenda . Hatutakuwa nchi ya kupewa handouts forever. Miaka 51 imepita toka tupate uhuru. Hatutaki ukoloni mambo leo bwana. Waache wakae na pesa zao. Cuba, imewekewa vikwazo miaka mingi, lakini wanao the best educated workforce, best and most doctors than hata Marekani. Nyie ACT msiwe vibaraka!
mdau 7:53 kweli unasizia, hvi unafananisha mbingu na ardhi, cuba sio tanzania, huo ni mfano wa mtoto anaejifundisha kutamba na tule anaekwenda shule. taanzania bado inahitaji kusaidia, miaka hamsini tangu tujitawale hatuna ha uwezo wa bajeti tegemezi, vyanzo vyote vya uchumi ni vile vilivyoacha na wakoloni, elimu baada ya kupanda kwetu inashuka, cuba itazalisha madaktari sisi tutazalisha vibaka kwa sababu hatuma mfuma madhubuti wa elimu
Bwana Kumwenda acha kushabikia nchi ambayo ni kigeugeu na wala haiithamini nchi yetu. Kama wenyewe kweli ni watetezi wa haki na demokrasia na hivyo misaada yao inatolewa kwa vigezo vya kutimiza masharti haya mbona muda siyo muda mrefu tu barani kwetu Afrika hivi majuzi dunia nzima ilishuhudia kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wa nchi yake na kwa kura nyingi lakini akapinduliwa na jeshi baada ya muda siyo mrefu na hawakusitisha misaada yao kwa nchi hiyo na badala yake misaada zaidi ndiyo inazidi kutiririka! Pia kuna nchi ambazo hazifikii hata hiyo demokrasia tuliyonayo Tanzania kwa ajili ya kukiukwa haki za binadamu na pia haziruhusu wanawake kupiga kura au hata kuendesha magari lakini bado zinaendea kuwa wafadhiliwa wakubwa wa nchi hii. Au ndiyo demokrasia mnayoisema ni ile ya watu wote ni sawa ila wengine ni sawa zaidi ya wenzao! Tuwe waangalifu wakati tunashabikia mambo. Nchi hii unayoishabikia hapa haina urafiki na nchi yetu hasa ikijuwa kuwa haina kitu itakayotarajia kupata kwetu. Napenda tu kuwakumbusha Watanzania wenzangu yale Baba wa Taifa aliyotuasia. Mwalimu wakati huo alisema nchi yetu iko tayari kupokea msaada kutoka kwa mtu au nchi yoyote hata kama ni kutoka kwa shetani ili mradi msaada huo hautaambatana na vikwazo au masharti yoyote. Tanzania ni nchi tajiri na kama Watanzania tutafuata maagizo tunayoagizwa na viongozi wetu hakika tunaweza kujikomboa katika makucha haya ya wanyonyaji na hivyo kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo a nchi yetu kwa nguvu zetu wenyewe hata bila msaada. Naamini kabisa kuwa tunaweza kama tukiamua kufanya hivyo na itakuwa vizuri kama tutawaacha hawa wenye misaada yao wake nayo wao wenyewe.
Kumbe Chama hiki hakina mwelekeo wa kisiasa wao ni kufuata wakubwa tu. Hivi uzalenfo hakuna tena ama ni ujinga unatawala watu na vyama vinavyojiita vya kisiasa.
Serikali ya Egypt iliyochaguliwa ki-demokrasia ilipinduliwa na Jeshi na utawala wa Kijeshi ukaitisha uchaguzi wa danganya toto. Serikali hiyo ya Kijeshi pia imevikandamiza haswa vyombo vya habari ikidai usalama! Licha ya yote hayo kando ya Israel, Egypt ni nchi ambayo bado inaongoza kupata matrlioni ya misaada ya Marekani.
Hayo yote hawa jamaa wa ACT hawayaoni ama ni kukosa kutambua kwamba mchezo hapa ni siasa tu. Hebu tuweke uzalendo wetu mbele tusikimbie tu kuwafurahisha wakubwa ili tupewe misaada bila kujali heshma na uhuru wetu.
Mhe Kumwenda nenda tu na bango pale Ubalozini ukaombe msaada wa Chama chako. Usitudhalilishe wote kwa kutaka utambuliwe na hao jamaa ili wakupatie msaada. Kaombe tu kama wengine wenzako walivyofanya.
Post a Comment