Advertisements

Thursday, March 31, 2016

BAADA YA WABUNGE WA CCM KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO KWA TUHUMA ZA RUSHWA, CCM YAFUNGUKA

Kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na tuhuma za baadhi ya wabunge kujihusisha na masuala ya rushwa.

Tuhuma hizo zimekuwa zikifanyiwa kazi na vyombo vya dola na kwamba tayari baadhi ya wabunge wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kinasikitishwa sana na tuhuma hizo, hasa pale zinapowahusisha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi  na kinaunga mkono jitihada za vyombo vya dola katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo.

Lazima ifahamike kuwa vitendo vya rushwa havina itikadi,dini, wala kabila na kwamba havikubaliki kwa namna yoyote kwani vina madhara makubwa kwa taifa.
CCM inavishauri vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua stahiki wabunge wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Chama cha mapinduzi kwa upande wake hakitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wabunge wake watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

1 comment:

Anonymous said...

Ooohhh how rotten is Bongoland, President Magufuli una kazi kubwa my new President. I think people are still in Awamu ya Nne which was rotten mpaka mfupa.

Viongozi wote was awamu ya nne wangeshitakiwa kwa kuiacha nchi imeoza.