Advertisements

Friday, March 4, 2016

BONDIA OMARI KIMWERI KUPANDA TENA ULINGONI APRIL 15 AUSTRALIA KUGOMBANIA UBINGWA WA DUNIA

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Omari Kimweri kupanda tena ulingoni April 15 nchini Australia katika ukumbi wa Melbourne Pavilion kwa ajili ya kugombania mkanda wa Dunia baada ya kumchapa
Michael Camelion wa Philippines kwa point
Bondia huyo Mtanzania mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia

amewashukuru watanzania kwa duwa zao walizo mwombea adi kufanikiwa kupata ushindi uliomwezesha kupata nafasi yakugombania mkanda wa Dunia
Kimweri mpaka sasa ameshacheza mpambano 18 akipoteza michezo 3
katika rekodi za ubora yeye ni namba 1 nchini
Australia na ni namba 98 katika rekodi za Dunia
bondia huyo anaetamba katika anga zakimataifa kupitia mchezo wa masumbwi Duniani amendelea kuomba watanzania kuwa waendelee kumuombea duwa na ato waangusha kamwe

kwa kuwa yeye ni mtanzania na kitovu chake kimezikia Tanzania kwa hiyo anajivunia utanzania wake akiwa ugaibuni

Kimweri alitoa shukrani za kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila 'Super D'

Kocha wa Tanzania Prison Remmy Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga

ambao amekuwa chachu katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama anaishi nje ya Tanzania

No comments: