ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 10, 2016

BREAKING NEWS: SAED KUBENEA AKAMATWA, AUNGANISHWA KWENYE KESI YA MDEE

Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amekamatwa na Jeshi la Polisi kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, baada yake kujumuishwa kwenye kesi ya Shambulio la Kudhuru Mwili inayowakabili wabunge wengine wa CHADEMA, Halima Mdee, Mwita Waitara na madiwani kadhaa wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam.

ENDELEA KUTUFUATILIA KWA TAARIFA ZAIDI

CHANZO: JAMII FORUMS

3 comments:

Anonymous said...

CCM tuavheni kuhujumu viongozinwaliowekwa na wananchinkwa maendeleo yao. Polisi inaacha kifuatilia wezi hadi kwenye mabenki wanapoteza muda kumsaka Kubenea!! Wanalipwa mshahara kuwafuatilia wapinzani ndicho kilichobaakia!! Hapo hakuna kesi ya kujibu wasakeni wezi na wala rushwa!--

Anonymous said...

Nini kesi ya kushambulia mwili!? Hebu mkamateni Mmbando aliyeanzisha hizo fujo na ndio kweli tutaelewa kazi inayofanyika. Avheni udhalilishaji..

Anonymous said...

Busara itumike huyo fala mnaemtetea yeye hajachaguliwa na wananchi kuja kupambana na vyombo vya dola kwa mambo ya hovyo. Kuna mambo mengi sana ya msingi yanayowakabili watu wake ambayo angeyashughulikia na kuleta manufaa zaidi kuliko kuanzisha bifu na serikali kabla hata hiyo kazi yake ubunge hajaianza. Kipindukipindu, ujambazi,Elimu kwa watoto hasa wanaoanza mwaka kwani huu ni mwanzo wa mwaka ni vizuri kujua kama madara yana tosha au hapana,walimu wanatosha au hapana,je vipi suala la elimu bure linaendelea vipi na changamoto zake? Kuna mambo kibao ya mtu mwenye kujua kipi cha msingi kupagania kwa ajili ya manufaa ya watu wake badala ya kuanzisha vita na serikali. Yeye kubenea fitna za CCM ataziweza wapi hicho chama kimezikomboa karibu nchi zote za kusini mwa bara la Africa au yeye alikuwa hajazaliwa kulifahamu hilo? Hata Nabii Musa alipoamriwa na Mungu kwenda kumwambia firauni aache ujinga wake wa kupotosha watu wake kuwa yeye ni mungu,lakini kabla ya Musa kunyanyua mguu wake kuelekea kwa Firauni kupeleka ujumbe uliompelekea kujenga bifu la kufa mtu na firauni,Mungu alimkubusha Musa juu ya cheo cha Firauni kama mkuu wa nchi na kumtaka kuwa na busara katika kuwasilisha ujumbe wake. Serikali not only in Tanzania but wherever, wheather you're right on your own rights or not, wisdom is indeed needed on dealing with it.