Saturday, March 5, 2016

DC -PAUL MAKONDA AZINDUA VITAMBULISHO VYA WALIMU KUPANDA DALADALA BURE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akimvika kitambulisho Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina Dar es Salaam leo asubuhi, baada ya kuvizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wa kwenda kazini kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao.
DC Makonda akimfika kitambulisho Mwalimu Gideon Mwenenyi.
DC Makonda akimvika kitambulisho, Mwalimu Ramadhani Korowelle.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wananchi na walimu wakati wa uzinduzi wa vitambulisho hivyo.
Ofisa Elimu wa Sekondari wa wilaya ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Turiani, Alpherio Nchimbi (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Walimu na viongozi wengine wakiwa kwenye hafla hiyo
Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mwalimu Happyness Mailo (kushoto), akimshukuru DC Makonda kwa kuwawezesha mpango huo.
Mwakilishi wa wananchi, Ahmed Muhonga akimshukuru DC Makonda.
Mshairi,  Msafiri Himba akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina akitoa neno la shukurani kwa DC Makonda.

Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua vitambulisho vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wakitoka nyumbani kwenda kazini.

Katika hatua nyingine Makonda ameziomba sekta mbalimbali nchini kushiriki katika kutoa mawazo yao ya maendeleo ili taifa lizonge mbele badala ya kuwa watizamaji.

Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana mbele ya wazazi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wakati akizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu wa wilaya yake kupanda daladala bure kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia  walimu hao.

"Nawaomba watanzania na sekta mbalimbali kuwa na mawazo ya maendeleo ambayo yatawekwa mezani na kuyafanyia kazi jambo litakalo msaidia Rais wetu Dk.John Magufuli katika kuliinua taifa kiuchumi badala ya kumuachia kila kitu akifanye yeye" alisema Makonda.

Makonda alitoa mwito kwa makondakta wa daladala kutoa ushirikiano kwa walimu hao kesho wakati watakapoanza kupanda magari yao huku wakijua walimu ndio waliowafundisha na kufikia hatua hiyo ya kazi walizonazo.

Ofisa Elimu wa Sekondari wa Wilaya hiyo, Rogers Shemwelekwa aliwaomba wananchi hao na walimu kuendelea kuunga mkono jitihada za Makonda za kuwaletea maendeleo na kumuombea kwa mungu badala ya kumbeza kwani kazi hizo anazozifanya ni kwa ajili ya wananchi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

1 comment:

Anonymous said...

Hongera kutoka kwa mdau wa New York city kwako ndugu Makonda,hongera sana kwa uthubutu wako. Tunasema siku zote kusoma sio kuelimika. Kuna wasomi wanaojiita wasomi siju kama wamemezwa na hulka za kisiasa au vipi. Katika maisha ya mwanadamu hawezi kupanuka kimawazo kama hatakumbana na challenge au changamoto katika maisha. Na ndio maana tunaambiwa tabibu bora za kutibu maharaha na upasuaji kwa haraka zilianzia vitani. Kwa maana ya kwamba daktari anapoamua kumtibu majeruhi vitani ilibidi atumie akili ya zaada kutokana na mazingira magumu yaliyomkabili. Wakati daktari akiumiza kichwa chake vipi ataweza kumtibu majeruhi wake vitani kwa haraka zaidi na ufanisi bila ya kujitambua kuwa wakati huo huo huyo daktari yupo kwenye njia ya kutafuta usuluhisho wa tiba bora kwa vizazi na vizazi vijavyo sio kwenye vita bali hata katika maisha ya kawaida. Ndugu Makonda ni mpambanaji kwa vitendo sio blah blah. Kupotea njia ndio kujua njia ingawaje siwezi kuita anayoyafanya muheshimiwa Makonda ni kupotea njia hapana,yeye ni mtu wa kutafuta usuluhusho wa wamatatizo katika yale masuala muhimu yatakayoipelekea nchi yetu kusonga mbele . Nani asiejua umuhimu wa elimu katika jamii yeyote ile? Na nani asiejuwa kuwa walimu wetu Tanzania wapo underpaid licha ya kazi kubwa na muhimu ya ajira yao? Nna hakika kabisa hata kama hili suala la kuwapatia walimu usafiri bure litatokezea kuwa kikwazo tayari kabisa msingi wa dhati wa kulitafutia ufumbuzi kero za usafiri kwa walimu uneshaasisiwa kitakachotafutwa ni maboresho kama zilivyo changamoto katika suala la elimu bure kwa wanafunzi, ni maboresho tu ili kuieka system sawa. Wale wanaobeza hizi jitihada ni ma cowards na wenye nia mbaya ya kuwavunja moyo wale wote watanzania wazalendo wenye nia nzuri ya kutoa mawazo mazuri kimatendo kwa ajili kuharakisha maendeleo ya nchi. Tunaomba wale wote wenye mawazo ya kimaendeleo wawe raia wa kawaida au mtumishi wa umma wasisite kuwasilisha mawazo kwenye taasisi husika ikiwezekana hata kwa muheshimiwa raisi mwenyewe ili yafanyiwe kazi kama yataonekana yanafaa. Kwa mara nyengine hongera sana muheshimiwa Makonda nnaimani pongezi hizi utazipata na huko unakofanya ndio tunakosema kumuunga mkono muheshimiwa raisi kwa vitendo kwani kufeli kwa Magufuli ni kufeli kwa Tanzania na watanzania. Kwa hivyo umoja ni nguvu na majungu yasio na mshiko wowote ni Sumu ulio laaniwa na Mungu.