Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema amewataka walimu kuwa wabunifu na kutatua baadhi ya matatizo bila kusubiri msaada wa Serikali au taasisi binafsi.
Akikabidhi msaada wa tangi la maji, printa, madaftari, kalamu na kompyuta uliotolewa na Umoja wa Watu wa Bengali (Bango Sangho) nchini India kwa Shule ya Msingi Kibugumo, Kigamboni, Mjema alisema ni vema walimu wakabuni miradi ili kumaliza baadhi ya changamoto.
“Wilaya yetu bado ina uhitaji wa madarasa 2,891 na madawati 28,000,” alisema.
Mwenyekiti wa umoja huo, Kunal Banerjee alisema wametoa msaada huo na huduma ya kupima afya bure kwa kutambua umuhimu wa afya na elimu kwa maendeleo ya sasa na baadaye kwa Taifa.
“Sisi tunapenda kuona hali nzuri ya elimu na tumeshasaidia kwa muda shule hii, tumetoa madawati 100 na tulijenga madarasa mawili na leo tumeleta msaada mwingine,” alisema Banerjee.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment