Bakari ni miongoni mwa majeruhi sita waliolazwa Taasisi ya Mifupa Moi, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiendelea kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali iliyohusisha daladala yenye namba ya usajili T629 CRT aina ya DCM, lori la mchanga na gari alilokuwa akiendesha lenye namba za usajili T109 DDX na kuua watu wanne na wangine 25 kujeruhiwa.
Akisimulia mkasa huo jana, katika wodi ya majeruhi ghorofa ya kwanza iliyopo jengo jipya, Jafari alisema wakati ajali hiyo ikitokea aliiona na akajaribu kuikwepa bila ya mafanikio.
“Nilivyokuta ajali ilibidi nianze kuwakwepa, kweli nilijitahidi nikawakwepa, lakini ile DCM ilinivaa hivyo kugongana nayo uso kwa uso, ndipo nami nilipoteza fahamu,” alisimulia huku akipumua kwa tabu.
Jafari ambaye ameumia zaidi maeneo ya kichwani, kifuani na mkono wake wa kulia, alisema alibanwa na usukani wakati akijitaidi kukwepa ajali ile.
Alisema baada ya kupoteza fahamu alishtuka wakati ameshaokolewa na wasamaria wema ambao waliomtaka ataje namba za ndugu zake ili wapatiwe taarifa za ajali hiyo.
“Kweli kwa wakati ule nilikumbuka namba ya shangazi yangu, aliyeko mkoani Dodoma na dada yangu aishie Mbagala ambaye walimpigia na kuwaeleza taarifa hizo,” alisema.
Alisema pia abiria aliokuwa nao kwenye gari hakuwaona tena na wala hafahamu hali zao na mahali walipo hadi sasa.
“Kwenye gari tulikuwa wanne tumekaa mbele, ambao ni wenye zile ng’ombe waliokodi gari na wawili nyuma walikuwa wakiswaga ng’ombe ili wasichoke kabla ya kufika mnadani, lakini baada ya ajali sijui hata mmoja yuko wapi,” alisema.
Alisema baada ya hapo hakujitambua hadi alipojikuta yuko hospitali akipatiwa matibabu.
Alisema katika ajali hiyo alipoteza fedha zake kiasi cha Sh. 300,000 alizokuwa nazo mfukoni na simu
NIPASHE
No comments:
Post a Comment