Saturday, March 5, 2016

DK.SHEIN ATEMBELEA MASKANI YA KISONGE ZANZIBAR

Kontena la Maskani ya kisonge Mjini Unguja laripiliwa kwa bomu na watu wasiojulikanwa usiku wa jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shei akipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Maskani ya Kisonge John Mwakanjuki leo wakati alipotembelea maskani hiyo baada ya kupata hasara kubwa ya mripuko wa bomu na watu wasiojuilikanwa usiku wa jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiangalia hasara iliyopatikana katika Maskani ya Kisonge iliyotokea jana kwa mripuko wa bomu uliosababishwa na watu wasiojuilikanwa, (wa pili kushoto) John Mwakanjuki alipotoa maelezo zaaidi kuhu tukio hilo leo wakati alipotembelea maskani hiyo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akizungumza na wanachama wa CCM na wapenda amani wakati alipofika katika Maskani ya Kisonge Mjini Unguja leo kuangalia hasara iliyopatikana kutokana na mripuko wa bomu uliosababishwa na watu wasiojuilikanwa jana usiku,

4 comments:

Anonymous said...


Bomu lolote linaporipuka, kinacholeta madhara ni shockwaves za bomu hilo
shockwaves za bomu ni mfano wa tone la maji linapodondoka kwenye maji yaliyotulia....yaani zinaanzia kati na kuenea kila upande kwa mfumo wa duara (circle)
Au kwa lugha ya kitaalam ni perimeter......
Hivyo, shockwave zinaweza kuleta uharibifu zaidi kulingana na aina ya kitu kilichopo karibu na ground zero (blast point)
Kontena la Kisonge limeonekana kuchanika kutokea ndani kuelekea nje.......
Hasa upande wa mlangoni mwa kontena hilo.....hii ina maana kuwa blast point ilikuwa ni ndani ya kontena, na kilichoharibu hilo kontena ni shockwave kutokea ground zero....
Ingekuwa blast point ni nje ya kontena, basi kontena lingebonyea kwa ndani.....
Kwa hiyo hii ina maana mbili.....1. hilo bomu limeingizwa humo ndani 2. Mlango wa kontena hilo daima hukomewa kwa kufuli kwa sababu wanalitumia kama ni stoo yao.....
Wataalam wa kutegua mabomu wanapaswa kwanza kuwahoji washika funguo wa hilo kontena kabla hawajaanza kuleta tafsiri nyengine maana facts zinaonyesha kuwa ni hujuma zilizofanywa na hao wenye dhamana ya hilo kontena...

Anonymous said...

mafisiemu wanafik sana mungu sasa one anawaubua ahsante mdau hapo juu kwa ufafanuzi.mwaka huu mtarimbo umewakanda hamchomoki

Anonymous said...

hivi hii nyumba au banda lililopigwa rangi ya kijani na bendera zake zinapepea ndio nini hii. Kweli CCM Imechoka, jingo gani hili na Rais wa kunyakua madaraka unaliona tangu umeingia madarakani hadi leo na bado wataka uendelee!! huu ni kudanganyana!!

Anonymous said...

Wachangiaji wawili wa mwanzo wa hapo juu nyote mnanuka harufu ya mwamsho na alshabibi. Unatoa ufafanuzi wako feki wa bomu jinsi linavyofanya kazi tungependa kufahamu hiyo taaluma umeipatia wapi? Na unaitumia kwa kazi gani? Na your location kwani kama utakuwa Zanzibar itakuwa vizuri kuuelimisha maamlaka husika kuwa hilo halikuwa bomu kutokana na taaluma yako utasaidia sana Amin. Hata hivyo jahazi linapo anza hitilafu hata kama wewe humo chomboni yawezekana ndugu,rafiki,jirani au waumini wenzio wamo mle ndani ya chombo si vizuri kuanza kutoa maneno ya kejeli kwani mara nyingi Mungu humpa mtihani kwanza yule anaemuombea mabaya mwenzio yamfike .